Viongozi wa Dini wakitoa heshima za mwisho
Watawa wa Kanisa Katoliki wakitoa heshima kwa Mwili wa Marehemu Dkt.Sengondo Mvungi.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa marehemu, Dkt.
Sengondo Mvungi, wakati wa shughuli ya kuaga mwili huo iliyofanyika leo
kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Waziri
Mkuu,Mh. Mizengo Pinda, akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye
mwili wa marehemu, Dkt. Sengondo Mvungi, wakati wa shughuli ya kuaga
mwili huo iliyofanyika leo kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es
Salaam.
Mamia
ya wakazi wa jiji la Dar es salaam pamoja na viongozi mbalimbali
wamejiokeza kutoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa mjumbe wa tume ya
mabadiliko ya katiba Dk.Sengondo mvungi aliyeuawa na watu
wanaodhaniwa kuwa ni majambazi huku serikali ikitakiwa kuhakikisha
inatafuta ufumbuzi wa kina wa kukomesha matukio kama hayo kwa raia wake.
Licha
ya kuwepo na mvua kubwa katika viwanja wa Karimjee waombelezaji hao
walishiriki katika shughuli za kutoa heshima za mwisho sambamba na ibada
maalum iliyoongozwa na Monisinyori Deogratius Mbiku,Paroko wa Chuo
Kikuu cha Dar es salaam ambaye amesema kila mtu atakufa na hivyo ni
bora wajiandae.
Akitoa
salamu za rambirambi Mwenyekiti wa NCCR -Mageuzi Mh.James Mbatia
amesema matukio kama haya yamekuwa yakitokea kila mara huku serikali
ikitoa ahadai ambazo hazitekelezeki hivyo muda umefika ichukue hatua.
Aidha
mwenyekiti wa tume ya marekebisho ya katiba Mh jaji mstaafu Joseph
Warioba amesema tume imepata pigo kubwa huku profesa paramagamba kabudi
akisoma wasifu wa marehemu ambapo amesema marehemu alikuwa ni sauti
ya kwanza kudai katiba mpya.
Makamu
wa rais Dk Gharib Bilal ni miongoni mwa viongozi wa serikali
waliokuwepo katika msiba huo ambapo kwa niaba ya rais ametoa salamu za
serikali ambapo amesema Dk Mvungi ameondoka wakati nchi bado inahitaji
mchango wake.
Kwa
upande familia ya Mvungi wameshukuru kwa namna ambavyo jamii
imejitolea katika msiba wa mpedwa wao na kwa hali hiyo wamesema
wamefarijika sana na kumwelezea baba yao kama mtu ambaye hakuwa muoga
na aliweka mbele utaifa huku baadhia ya waombolezaji wakieleza namna
marehemu alivyokuwa na mchango mkubwa wa jamii hasa vijana waliokuwa
wanasoma masomo ya sheria
0 comments:
Chapisha Maoni
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.