Searching...
Jumapili, 24 Novemba 2013

HII HI YA SASA HIVI, SOMA ALICHOKISEMA ZITTO NA DKT. KITILIA KWA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU KUVULIWA MADARAKA NA CHADEMA

 
Aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu Chadema, Dk Kitilia Mkumbo amekiri kwamba alishirikiana na Samson Mwigamba katika kuandaa waraka wa mabadiliko katika Chama hicho, lakini siri hiyo iilivuja baada ya Mwigamba kukamatwa na kunyang'anywa Laptop ambayo ilikuwa na wakara mzima.
 
Dk Kitilia amefafanua kwamba sababu ya yeye kuandaa waraka huo ilikuwa ni kuleta mabadiliko ndani ya Chama hicho. Kwa upande wake Zitto Kabwe anasema kwamba yeye hawezi kuwa chanzo cha Chadema kufa na kamwe hawezi kukivuruga Chadema kwamba ndicho kilicho mlea.
 
"Nilijiunga Chadema nikiwa na miaka 16, hivi sasa nina miaka 37, ningependa siku moja mtoto wangu aje kuwa mwanachadema, kuna tuhuma nyingi sana juu yangu ambayo kimsingi sikuhusika nayo hata kidogo.
 
Tuhuma kubwa iliyochukuwa nafasi kubwa na muda mwingi katika mkutano wa Kamati Kuu,ni tuhuma za Kamati ya Bunge na Hesabu za Serikali kusema kwamba Chadema haijawasilisha hesabu zake kwa CAG, lakini nikaambiwa kwamba nilipaswa kuwatonya viongozi wa Chadema kabla ya kutangaza hadharani hivyo nikaambiwa kwamba nimekidhalilisha Chama".
 
"MImi nikiwekewa chaguo la nchi na Chama nitachagua nchi kwanza si Chama, hivyo nilifanya vile kwa muujibu wa taratibu za kamati yangu"

"Tuhuma nyingine nikaambiwa kwamba mimi ni mnafiki kwa kukutaa kuchukuwa posho za vikao vya bunge"..

"Mimi sitoki Chadema, na wanaotaka nitoke wanitoa kwa njia wanaotaka wao,na nitakuwa wa mwisho kutoka, nimefanya kazi kubwa ndani ya Chadema,ninapotuhumiwa ninaumia, tuache siasa za chuki.

Bado  anaendelea..

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!