MBUNGE WA UKEREWE MH.SALVATORY MACHEMLI.
Juhudi za kumdhamini Mbunge wa Ukerewe,
Salvatory Machemli (CHADEMA), aliyewekwa mahabusu kwa siku ya nane sasa,
zimekwama. Kaimu Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Ukerewe, Mrisho Abed,
alisema jana kuwa amri ya kumweka Machemli rumande kwa siku 14 ilitolewa
baada ya mshitakiwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.Alisema Sheria ya Makosa ya Jinai namba
20 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002 imeipa Mahakama mamlaka ya kufuta
dhamana ya mshitakiwa.
Hawa Chadema wanaubaguzi wa kikanda, kweli huyu jamaa angekuwa wa Kaskazini au mchagga wangemuacha asote rupango siku zote hizi? mbona kipindi "fulani" waliandamana na kulala nje, walituma mawakili 10 kudogo kwenye kesi ya mtu "fulani" ? Wanaona sisi "yego" hatuna thamani?
JibuFuta