PICHA NA MAKTABA
Taarifa ambazo zimetufikia hivi punde kutoka visiwani zanzibar zinasema jeshi la polisi kwa kushirikiana na vikosi maalumu wamefanikiwa kukamata kontena lenye ukubwa wa futi 40 likiwa limesheheni meno ya tembo ambayo mpaka hivi sasa idadi yake haijafahamika.
akizungumza na waandishi wa habari katika bandari ya zanzibar waziri wa ofisi ya Rais Tawala za mikoa,Idara Maalumu na vikosi vya SMZ mheshimiwa HAJI OMARY HERI amesema kiwango cha meno hayo ni kikubwa na kutokana na tukio hilo ilimlazimu waziri wa maliasili na utalii mheshimiwa Balozi Hamis Kagasheki kufunga safari ya ghafla na kutua visiwani humo kushuhudia tukio hilo la kusikitisha.
hadi mawaziri hao wanazungumzia tukio hilo bado zoezi la kuhesabu meno hayo lilikua linaendelea.
kwa taarifa zaidi kuhusu tukio hili,nani alihusika,meno yalikua ni mangapi,yalikua yanapelekwa wapi,ikiwa ni pamoja na picha endelea kutembelea MCHOME BLOG
0 comments:
Chapisha Maoni