MWANAFUNZI
mmoja ameuawa kwa kipigo na mwili wake kutupwa kichakani akituhumiwa
kuiba maandazi. Mwanafunzi huyo (jina limehifadhiwa) alikuwa akisoma
darasa la pili katika Shule ya Msingi Nyakadete, iliyopo wilayani
Mbarali mkoani Mbeya.
Kaimu
Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya, Robert Mayala, alidai kuwa mwanafunzi
huyo mkazi wa Kijiji cha Nyanyembe Kata ya Madibira, aliuawa kwa kupigwa
na kisha mwili wake kutupwa vichakani akituhumiwa kuiba maandazi.
Kamanda
Mayala alidai mwili wa mwanafunzi huyo ulikutwa Jumatatu saa 4:00
asubuhi, ukiwa kichakani katika Kijiji cha Unyanyembe Nyamakuyu Kata ya
Madibira.
Kutokana
na tukio hilo, polisi wanamshikilia Edmund Kwinge (30) mkazi wa Kijiji
cha Nyakadete, akituhumiwa kuhusika na mauaji ya mwanafunzi huyo na
atafikishwa mahakamani mara baada ya uchunguzi kukamilika.
0 comments:
Chapisha Maoni