Searching...
Alhamisi, 24 Oktoba 2013

WATU 38 WAJERUHIWA VIBAYA KATIKA AJALI ILIYOHUSISHA MAGARI 4 IRINGA

Daladala aina ya Coster lenye namba za usajili T.960 AQY  inayofanya safari zake za Kibwabwa mjini Iringa mara baada ya kugongana na gari aina ya Isuzu Tipa, lenye namba SM 3363 katika  Mlima wa Ipogolo eneo la Kisima cha Bibi.    
 Taxi ambayo nayo ilisababishiwa ajali ikiwa katika eneo la tukio, huku askari polisi wakilinda usalama wa mali za abiria na baadhi ya vitu katika eneo la tukio.
====
ZAIDI ya abiria 30 wamejeruhiwa katika ajari iliyohusisha magari manne mjini Iringa, baada ya Bus dogo la abiria aina ya Coster kufeli breki na kuyagonga magari matatu, ajali ambayo imetokea majira ya saa saba mchana wa siku ya Jana.
Tukio hilo limetokea  katika mlima wa Ipogolo, eneo maarufu mjini Iringa kama "Kisima cha bibi", ambapo ajali hiyo imesababisha majeruhi 38 ambao wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa mkoani Iringa, huku chanzo cha ajali hiyo kikisemekana kuwa na kufeli breki kwa Bus hilo la abiria,lenye namba T. 960 AQY na kuyavaa magari matatu, gari kubwa aina ya Tipper Isuzu SM784 BNA la manispaa ya Iringa,  Tax pamoja na Hiace.
Akizungumzia hali ya majeruhi wa tukio hilo , Mganga mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa mkoa wa Iringa Dr. Deogratius Manyama amesema wamepokea majeruhi 38, na waliolazwa ni 8 huku majeruhi watatu wakiwa na hali mbaya, na kuwa majeruhi wengi wameumia zaidi  kichwani na kifuani, huku majeruhi 27 wakiruhusiwa kurudi nyumba kwao kutokana na kutokuwa na majeraha makubwa.
 na OLIVER MOTTO

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!