Searching...
Jumatano, 23 Oktoba 2013

MUNGU AWAUMBUA FREEMASON,MUUMINI WAO AOKOKA,ATOBOA SIRI YA KUKATWA KIDOLE

Aliyekuwa Freemason kwa miaka 14 afunguliwa katika mkutano wa Ufufuo na Uzima unaoendelea Moshi; alikatwa kidole akiwa mdogo kama udhihirisho wa alama yao (devil horns)
alieleza mwenyewe mbele ya waliokuwepo mkutanoni maelfu ya watu wa mkoa wa Kilimanjaro na vitongoji vyake wanaohudhuria mkutano huo katika viwanja vya mashujaa unaoongozwa na mchungaji Josephat Gwajima wa kanisa la Ufufuo na Uzima lenye makao makuu yake Kawe jijini Dar es salaam.
Binti wa kiislamu ambaye aliwekwa ndani ya bahari kwa miaka mingi; alipokea ukombozi wake mara baada ya maombezi. Kule baharini alikuwa ameolewa na jini ambaye alimweka awe malkia wa baharini kwa miaka mingi... Mungu akamrudisha baada ya maombezi na kumpokea Yesu Kristo.
Njia ni moja tu nayo ni YESU, askofu Gwajima akifundisha mkutanoni.
Flora Mbasha na mumewe wapo sambamba na wana Ufufuo na uzima mkoani Kilimanjaro.
Mchungaji kiongozi Josephat Gwajima akiowaongoza kwa maombi wakazi wa mkoa wa Kilimanjaro.

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!