Ghati Chacha (21) mkazi wa kijiji cha Nyanitira kata ya
Nyansincha Wilayani Tarime amesababishiwa kilema cha maisha kwa kukatwa mguu
wake wa kulia na Mume wake baada ya kuchelewa kumfungua mlangao nyakati za
usiku.
Akisimulua mkasa huo hivi karibuni akiwa wodi namba sita alikolazwa akiuuguza vidonda na
majeraha,Ghati alisema, mume wake aliye
mtaja kwa majina ya Chacha Mwita(23) alifika nyumbani saa mbili usiku akiwa
amelewa.
“Aliniuliza kwa nini nimechelewa kumfungulia mlango nikamjibu
sikuwa nasikia, baadaye akaniomba kurunzi na panga, nikamletea kurunzi na kumwonesha
panga lilipo kwa kidole” alisema Ghati.
Wakati anamwonesa lilipo panga na kumpa kurunzi Ghati
hakujuwa kuwa nini kinafuata alifiki
kuwa mambo ya wanaume pengine anataka kwenda
sehemu kwa kuwa ndizo tabia za wanaume wa maeneo haya kuondoka usiku ama
anataka kuangalia mji kama uko sawa alafu arudi kulala.
“ Alipoipata ile panga akaniambia leo atamitumbua utumbo,
akaanza kunipiga kwa panga ile
akanijeruhi sikio, mkono wa kushoto na mguu wa kushoto na kunikata mguu wa
kulia ukakatika kama unavyoona” alieleza
kwa masikitiko akiifunua kanga iliyokuwa amejifunika akiwa amelala
kitandani hospitali ya Wilaya Tarime.
Wakati anafanyiwa ukatili huo ali piga kelele lakini
majirani hawakuwahi kufika kumsaidia kwa
kuwa ni kawaida ya mume na mke kugombana na vilio kama hivyo kusikika katika
maeneo hayo.
“Baadaye walikuja na aliposikia majirani wamefika alikimbia
kwa kupitia mlango wa nyuma akitumia baisikeli yake, majirani walinifunga mguu
uliokuwa ukivuja damu na kunikimbiza katika kituo cha afya Muriba na baadaye
kuletwa hapa” alieleza .
Hata hivyo mwanzoni Ghati alieleza kuwa chanzo cha matatizo
hayo yote ni ndoa za mitala na unywaji wa pombe wa mume wake.
“ Nimeishi naye kwa miaka mine sasa na tuna watoto wawili na
tulikuwa tunaishi vizuri, tatizo akinywa pombe huonekana kama amewehuka linguine
ni baada ya kuoa mke wa pili ambapo
alianza kunichukia , kuanza kunipiga na sasa kunikata mguu” alisema Ghati.
Ghati hataweza
kurudiana na mume wake huyo kwa kitendo
alichomfanyia kwa vile amesema hakioneshi utu na kuiomba mahakama imuhukumu
mumewe kifungo jera ili ajifunze
kutokana ukatili aliomfanyia.
” Naomba serikali na watu binafsi wanisaidie magongo ya
kutembelea kwa kuwa sasa sina uwezo wa kuyanunua pia wanisaidie kusomesha
watoto wangu maana ni wadogo na mimi ndiye niliye kuwa nikitafuta tunakula”
alisema.
Wananchi walioshuhudia kitendo hicho walionesha
kusikitishwa na kukilaa kuwa kinaendelea
kuharibu jina la na sifa ya Wilaya ya Tarime .
“ Sikifurahii kitendo hiki kwani kinaonesha wazi ukatili wa
hali ya juu kwa binadamu mwenzako na hii
inasababisha hata watu ambao hawajawahi kufika huku kutuona sisi ni
wanyama kumbe ni watu wachache wanaotuharibia sifa, mahakama imuhukumu huyu mtu
adhabu kubwa inayomstahili ili liwe
fundisho kwa wengine” alisema Mwita Machera aliyekuwa hostalini hapo.
Jeshi la polisi baada ya kupata taarifa lilifika lilifika
eneo hilo la tukio na kushuhudia kipande cha mguu kama inavyoonekana kwenye
picha hapa na kuamru kizikwe na juhudi za kumtia nguvuni kuanza.
Hata hivyo siku mojs baadaye Chacha Mwita alikamatwa na
jeshi la polisi kwa kusaidiana na nguvu nza wananchi ambapo alifikishwa katika
mahakama ya Wilaya ya Tarime kujibu mashitaka hayo.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamishina masaidizi wa
polisi kanda maalumu ya Tarime (ACP) Justus Kamugisha lisema kuwa baada ya
kuhojiwa Mwiata alikiri kumsababishia mke wake ukilema wa maisha.
“ Vitendo vya kikatili vilishapitwa na wakati,
kumsababishia mtu ukilema wa maisha sii jambo lisilo la utu na linaonesha kuwa hakuna
ubinadamu kwa watu japo si wote” alisema Kamugisha kwa nija ya simu.
Chanzo Dj sek Blog
0 comments:
Chapisha Maoni