ENZI HIZO FERGUSON ALIPOFUNGASHA VIRAGO VYAKE KUELEKEA KIJIJINI KUPUMZIKA BAADA YA KUSTAAFU.
Kocha wa Arsenal Arsene Wenger amezidi kukoleza uvumi kwamba kocha wa zamani wa Man u Sir Alex Ferguson huenda akarejea tena dimbani kuifundisha klabu hiyo kipenzi chake cha roho kufuatia muendelezo mbovu na matokeo ya kusikitisha inayopata timu hiyo,ambapo Wenger ameviambia vyombo vya habari kwamba hatoshangaa kumuona babu mwenzake Ferguson akirudia tena kibarua chake kabla ya mwisho wa msimu huu.

ARSENE WENGER NA BABU MWENZAKE
FERGUSON WAKISALIMIANA ENZI HIZO KATIKA MOJA YA MECHI WALIZOKUTANA ARSENAL NA
MAN U
Wenger, Ambaye amekiongoza kikosi hicho cha wabeba mitutu wa London Arsenal the Gunners tangu mwaka 1996, alichukua nafasi ya Ferguson kama kocha mkongwe katika ligi kuu England baada ya Mscotland huyo kustaafu ghafla mwishoni mwa msimu uliopita.
‘baada ya miezi sita tutajua kama Ferguson atarejea ama la,’ alimalizia Wenger.
BABU FERGUSONI ALIPOKUA AKIONDOKA KWENYE MAKAZI YAKE MANCHESTER BAADA YA KUSTAAFU.
HII NDIYO HELCOPTA ALIYOONDOKA NAYO FERGUSON...SWALI LINAKUJA,JEEE,ATAPANDA TENA HELCOPTA NA KUREJEA JIJINI MANCHESTER KUIOKOA MAN U NA AIBU INAYOINYEMELEAAA???????!!! TUSUBIRI TUONE
0 comments:
Chapisha Maoni