Searching...
Jumatatu, 28 Oktoba 2013

HIVI NDIVYO MBIO ZA ROCK CITY MARATHON ZILIVYOFANA.

Mshindi  wa kwanza wa mbio za Rock City Marathon 2013 kilomita 21 kwa upande wa wanaume Alphonse Felix kutoka mkoani Arusha akimalizia mbio hizo kwenye uwanja wa CCM Kirumba ambapo alitumia saa 1:02:17 na kufanikiwa kuvunja rekodi iliyowekwa mwaka jana na Opio Chacha aliyetumia saa 1:05:47.
Afisa Uhusiano na Masoko wa Mfuko wa hifadhi wa jamii NSSF  Bi. Theopista Mheta akimkabidhi zawadi ya shilingi 1,500,000/= mshindi wa kwanza mbio za Rock City Marathon kilomita 21kwa upande wa wanaume Alphonse Felix ambaye pia alijinyakulia zawadi ya tiketi ya ndege toka moja wa wadhamini wa mbio hizo Precission Air, ya kuelekea Dar es Salaam na kurudi mkoani kwake Arusha.
Afisa Mauzo wa King’amuzi cha Continental, Dominic Kiluma akikabidhi zawadi ya king’amuzi kwa Joel Kimbiaye toka Kenya mara baada ya kuibuka mshindi wa nafasi ya pili mbio za Rock City Marathon 2013 ambapo pia mshiriki huyo alijinyakulia kitita cha shilingi 900,000.
Afisa Mahusiano na Masoko wa Mfuko wa hifadhi wa jamii NSSF Bi. Theopista Mheta  akikabidhi zawadi ya shilingi 700,000/= mshindi wa tatu katika mbio za Rock City Marathon  kilomita 21, Andrew Sambu ambaye pia alijinyakulia king’amuzi cha Continental.
Afisa Uhusiano na Masoko wa Mfuko wa hifadhi wa jamii NSSF  Bi. Theopista Mheta akimkabidhi zawadi ya shilingi 1,500,000/= mshindi wa kwanza mbio za Rock City Marathon kilomita 21 kwa upande wa wanawake Vicoty Chepkemoi kutoka Kenya.
Afisa Uhusiano na Masoko wa Mfuko wa hifadhi wa jamii NSSF  Bi. Theopista Mheta akimkabidhi zawadi ya shilingi 900,000/= mshindi wa pili wa mbio za Rock City Marathon kilomita 21 wanawake Sarah Ramadhan ambaye pia alinyakuwa king’amuzi cha Continental.
Afisa Mauzo wa King’amuzi cha Continental  Dominic Kiluma akikabidhi zawadi ya king’amuzi kwa mshindi wa tatu mbio za Rock City Marathon 2013 wanawake, Zakia Mrisho ambaye pia alijinyakulia kiasi cha shilingi 700,000/=
Washiriki kutoka Australia wakimaliza mbio za kilomita 21.
Baadhi ya raia wa nchi za kigeni wakipumzika baada ya kumaliza mbio za Rock City Marathon
Meneja Uhusiano wa Airtel  Bw, Jackson Mmbando akimpongeza mshindi wa kwanza wa mbio za kilomita 2,  Benedicto Mashauri wa mwanza, baada ya kuwashinda watoto wenzake 284 walioshiriki mbio za Rock City Marathon 2013
Mkurugenzi wa Club ya Holili Youth Athletics iliyoko mkoani Kilimanjaro wilayani Rombo Domian Rwezaura Janand, akitamba mara baada ya mashindano kwa washiriki toka kambi yake kufanya vyema kwenye mbio za Rock City Marathon 2013
Sehemu ya watoto waliowakilisha walioshiriki mbio za Rock City Marathon 2013.
                              =======
WANARIADHA Alphonce Felix kutoka Arusha na Vicoty Chepkemoi kutoka Kenya wameibuka vinara katika mashindano ya riadha ya kilometa 21 yanayojulikana kama ‘Rock City Marathon 2013’ yaliyofanyika Jijini Mwanza jana Jumapili nakujinyakulia Shilingi milioni moja na nusu (Sh 1.5 m) kila mmoja.
Alphonce alishinda mbio hizo kwa upande wa wanaume baada ya kutumia saa 1:02:17 hivyo kuvunja rekodi iliyowekwa mwaka jana na mwanariadha Kopiro Chacha aliyetumia

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!