Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (kushoto) akiwa na Mwenyekiti wa
Baraza la Mawaziri wa Nchi za Maziwa Makuu na Pembe ya Afrika katika Mapambano
ya Kuzuia na Kudhibiti Uzagaaji wa Silaha Haramu (RECSA) ambaye pia ni Waziri
wa Mambo ya Ndani wa nchini Rwanda, Sheikh Mussa Fazil Harerimana wakiwa tayari
kuipokea bendera ya RECSA kabla ya Dk Nchimbi kukabidhiwa bendera hiyo ikiwa ni
ishara ya kukabidhiwa kuliongoza baraza hilo kwa kipindi cha miaka miwili.
Hafla ya makabidhiano hayo ilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya
Serena, jijini Dar es Salaam leo. Nchi wanachama wa RECSA ni Burundi, Congo,
Djibout, Ethiopia, Eritrea, Kenya, Rwanda, Sudan, Uganda na Tanzania.
JUU NA CHINI: Mwenyekiti
mpya wa Baraza la Mawaziri wa Nchi za Maziwa Makuu na Pembe ya Afrika katika
Mapambano ya Kuzuia na Kudhibiti Uzagaaji wa Silaha Haramu (RECSA) na Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi akizungumza na wajumbe wa Baraza
hilo pamoja na watendaji wakuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi pamoja na
wananchi mbalimbali baada ya kukabidhiwa uenyekiti huo katika hafla
iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Serena, jijini Dar es
Salaam leo. Nchi wanachama wa RECSA ni Burundi, Congo, Djibout, Ethiopia,
Eritrea, Kenya, Rwanda, Sudan, Uganda na Tanzania.
Mwenyekiti
mpya wa Baraza la Mawaziri wa Nchi za Maziwa Makuu na Pembe ya Afrika katika
Mapambano ya Kuzuia na Kudhibiti Uzagaaji wa Silaha Haramu (RECSA) na Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (kushoto) akimkabidhi zawadi
mwenyekiti aliyemaliza muda wake wa kuiongoza RECSA ambaye ni Waziri wa Mambo
ya Ndani wa nchini Rwanda, Sheikh Mussa Fazil Harerimana. Hafla ya makabidhiano
hayo iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Serena, jijini Dar es
Salaam leo. Nchi wanachama wa RECSA ni Burundi, Congo, Djibout, Ethiopia,
Eritrea, Kenya, Rwanda, Sudan, Uganda na Tanzania.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (kulia viti vya
mbele) akiwa na watendaji wengine wakuu wa wizara hiyo pamoja na wageni
waalikwa wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti mpya wa Baraza la Mawaziri wa Nchi
za Maziwa Makuu na Pembe ya Afrika katika Mapambano ya Kuzuia na Kudhibiti
Uzagaaji wa Silaha Haramu (RECSA) na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk
Emmanuel Nchimbi (hayupo pichani) mara baada ya kukabidhiwa uenyekiti wa RECSA
na Waziri wa Mambo ya Ndani wa nchini Rwanda, Sheikh Mussa Fazil Harerimana.
Hafla hiyo makabidhiano ilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Serena,
jijini Dar es Salaam leo. Nchi wanachama wa RECSA ni Burundi, Congo, Djibout,
Ethiopia, Eritrea, Kenya, Rwanda, Sudan, Uganda na Tanzania.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (kushoto) akipokea bendera ya Baraza
la Mawaziri wa Nchi za Maziwa Makuu na Pembe ya Afrika katika Mapambano ya
Kuzuia na Kudhibiti Uzagaaji wa Silaha Haramu (RECSA) kutoka kwa mwenyekiti wa
baraza hilo anayemaliza muda wake ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani wa
nchini Rwanda, Sheikh Mussa Fazil Harerimana. Dk Nchimbi sasa ni Mwenyekiti
mpya wa RECSA ambaye anaiongoza kwa kipindi cha miaka miwili. Hafla ya
makabidhiano hayo ilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Serena,
jijini Dar es Salaam leo. Nchi wanachama wa RECSA ni Burundi, Congo, Djibout,
Ethiopia, Eritrea, Kenya, Rwanda, Sudan, Uganda na Tanzania.
Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi.
KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.
0 comments:
Chapisha Maoni