GARETH BALE.
Agosti mwaka huu, Real Madrid, ilifanya kufuru baada ya kuvunja benki na kuandika historia mpya kwenye soka kwa kufanya usajili wa pesa nyingi zaidi duniani. Ni wakati walipomnasa winga wa Wales, Gareth Bale, kwa uhamisho wa Pauni 85 milioni.
Uhamisho ulikuwa gumzo Ulaya nzima na kuwafanya
watu wengine wafike mbali na kuchambua mambo mengine ambayo yangeweza
kufanywa kwa kutumia pesa hiyo ya usajili wa Bale.
Lakini hata mwaka ukiwa haujaisha, tayari Real
Madrid inaonekana kama imeingia mkenge kwenye usajili huo uliowagharimu
pesa nyingi.
Daktari asema Real Madrid imeliwa
Katika kusaka ukweli wa kitaalamu kuhusiana na
maradhi ya mgongo yanayomsumbua Bale, gazeti maarufu jijini Madrid,
MARCA lilifanya mahojiano na madaktari mbalimbali mahiri wa
Kihispaniola.
Wakamfuata daktari mwenye hadhi kubwa, Avelino
Parajon na akasema hivi: “Kama Real Madrid ilimsajili Gareth Bale
ikidhani kwamba hili ni tatizo dogo tu, wamefanya kosa kubwa sana.
0 comments:
Chapisha Maoni