Searching...
Jumatano, 30 Oktoba 2013

ANGALIA PICHA 5 NA MAELEZO KAMILI YA AJALI MBAYA YA TRENI ILIYOUA 11 JIJINI NAIROBI ASUBUHI YA LEO.

 Watu 11 wamethibitishwa kufariki katika ajali iliyohusisha treni na basi iliyokuwa imewabeba watu wakielekea kazini katika mtaa wa Umoja viungani mwa mji wa Nairobi.
 Basi hiyo inayoaminika kuwa na watu 34 iligongwa na treni kwenye njia ya reli kuelekea mjini. Kwa mujibu wa shirika la Red Cross, idadi ya majeruhi imefika 34 na wamepelekwa katika hospitali kuu ya Kenyatta.
 Baadhi ya waliojeruhiwa wanasemekana kuwa katika hali mbaya Walioshuhudia ajali hiyo wanasema kuwa basi hilo lilisukumwa umbali wa mita hamsini baada ya kugongwa kwa upande na Inaarifiwa watu sita walifariki papo hapo na wengine wawili kufariki baadaye kutokana na majeraha waliyoyapata.
 Wengine wengi wamejeruhiwa kwa mujibu wa shirika la msalaba mwekundu Mwandishi wa habari wa shirika la habari la AFP aliyeshuhudia ajali hiyo alisema kuwa basi iliharibiwa vibaya baada ya kugongwa kwa upande na treni ihiyo ilikuwa inasafiri kwa kasi kubwa.
Ajali hiyo imetokea asubuhi wakati wa msongamano wa watu na magari huku watu wengi wakiwa katika haraka kuu kuelekea kazini

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!