Mwili wa kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Rashidi Seleman mkazi
wa Isevya manispaa yaTabora ambaye amepoteza maisha baada ya Lori walilokuwawamepanda kuanguka eneo la Inala barabara ya kwenda Kigwa,Polisi wamesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa dereva ambaye amekimbia huku watu wengine wanne wakiwa wamejeruhiwa vibaya ambao wamelazwa katika hospitali ya Rufaa ya Kitete.
Tatizo
la ukosefu la ukosefu wa vifaa vya kuokolea vilisababisha maiti ya mtu
huyo kukaa muda mrefu akiwa amebanwa na Lori hilo ambalo ni mali ya
kampuni ya mkandarasi JOSSAMwa Isevya manispaa yaTabora ambaye amepoteza maisha baada ya Lori walilokuwawamepanda kuanguka eneo la Inala barabara ya kwenda Kigwa,Polisi wamesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa dereva ambaye amekimbia huku watu wengine wanne wakiwa wamejeruhiwa vibaya ambao wamelazwa katika hospitali ya Rufaa ya Kitete.
Awali
jitihada za Polisi na wananchi ziligonga mwamba na kubaki wakiiangalia
maiti hiyo pasipo msaada wowote ajali ambayo imetokea majira ya saa kumi
jioni hapo jana.
Askari
wa usalama barabarani wakiongozwa na kamanda wa Polisi kikosi cha
usalama barabarani wilaya ya Tabora Bw.Swaleh Digega hatimaye
wakafanikiwa kuutoa mwili wa marehemu huyo na kuupeleka hospitali ya
mkoa wa Tabora Kitete kwa ajili ya kuuhifadhi....Hata hivyo Jeshi la
Polisi kwa kushirikiana na Sumatra wanakusudia kumfikisha mahakamani
mmiliki wa Lori hilo kwa kitendo cha kusafirisha mizigo na wanadamu
katika gari hilo lenye nambari za usajili T 702 ACR ambalo ni ISUZU TX
0 comments:
Chapisha Maoni