Ajali mbaya
imetokea asubuhi majira ya saa 2 kwenye barabara ya majita karibu
na makazi ya mkuu wa mkoa wa Mara baada ya gari aina ya VX land cruser
namba T 901 AHH kuigonga pikipiki iliyokuwa ikitoka maeneo ya mjini
musoma kuelekea kamnyonge.
Kamera yetu
imemshuhudia majeruhi wa ajali aliyedaiwa kuwa ni abiria akiwa anavuja
damu nyingi kichwani huku akipumua kwa shida na muda mchache askari wa
kikosi cha usalama barabarani walifika eneo la tukio na kumchukua kwa
ajili ya kumuwahisha hospitali.
Mashuhuda
walioshuhudia ajali hiyo kabla ya camera ya blog hii kufika eneo la
tukio muda mchache wamesema dereva wa pikipiki ambaye alidaiwa kupakia
abilia alitaka kulipita gari hilo na kuingia eneo la gari hali
iliyopelekea kutokea kwa ajali hiyo.
Mmoja wa
mashuhuda wa ajali hiyo dereva wa pikipiki Wambura Matiku aliyekuwa
nyuma ya pikipiki iliyopata ajali aliiambia blog hii dereva wa pikipiki
mara baada ya kulipita gari hilo aliwahi kuingia upande wa gari na kutokea kwa ajali hiyo.
Hata hivyo
jeshi la polisi mara baada ya kumuwahisha majeruhi huyo hospitalini
walirejea eneo la tukio na kupima ili kubaini chanjo cha ajali hiyo huku
Kamanda wa polisi Mkoa wa Mara Ferdinand Mtui akiahidi kuhitolea
taarifa mara baada ya kubaini chanzo cha ajali hiyo
0 comments:
Chapisha Maoni