
Mwanadada
Shilole akionesha umahiri wake wa kunengua jukwaani mbele ya maelfu ya
watazamaji waliojitokeza usiku wa jana kwenye tamasha la Serengeti fiesta
2013.
Anaitwa Linah Sanga,kutoka nyumba ya vipaji THT akiimba jukwaani usiku huu
Watu
kibao,kila mmoja akijiachia kivyake huku jukwaa likiwaka moto vilivyo
kwa miondoko ya bandika bandua ya wasanii wanaotumbuiza.
Wakali
wengine wanaokuja kwa kasi katika anga la bongofleva-hip hop,Stamina na
Youngkiller wakilishambulia jukwaa kwa kushusha mistari mikavu live.
Shangwe kila kona za mashabiki zimetawala uwanjani hapa.
Msanii
wa muziki wa bongofleva ambaye kwa sasa anafanya vyema kwenye anga
hizo,Neylee akiimba jukwaani usiku wa jana wakati wa tamasha la serengeti
fiesta 2013 likiendelea usiku huu ndani ya uwanja wa Karume,Musoma
mkoani Mara.
Kundi
la Wanaume TMK Halisi likiongozwa na msanii nguli Juna Nature
wakilishambulia vyema jukwaa usiku huu kwa staili yao mapanga shaa
shaa,huku mayowe yakipigwa kutoka mashabiki.
Kila shabiki alikuwa na mzuka wake.
Mashabiki wa tamasha la serengeti fiesta wakifuatilia yanayojiri ndani ya uwanja wa Karume hivi sasa.
0 comments:
Chapisha Maoni
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.