Mtoto Shabani Maulidi akiwa tayari melala kitandani katika hospitali ya wilaya ya Geita.
Mama mzazi wa mtoto Shabani menye kilemba kichwani akiwa amepigwa bumbuazi maeneo ya hospitali.
Eneo ambalo mawe yanaonekana nyuma ya nyumba ndipo Mtoto huyo alipo zikwa
Wadogo zake na Shabani nao wakiwa wameshikwa na mshangao kama walivyokutwa nyumbani kwao.
........................
MTOTO
anayedaiwa kufariki miaka miwili iliyopita na kufanyiwa matanga
ameonekana akiwa hai Septemba 28 majira ya mchana baada ya kukutana na
mama yake mzazi uso kwa uso wakati akienda kwenye shughuli zake za
kibiashara.
Mtoto
huyo Shabani Maulidi (15) alifariki tarehe 03.01.2010 alishindwa kurudi
nyumbani kwao tarehe 01.01.2011 wakati alipokuwa amepeleka Mbuzi
machungani kisha kushindwa kurudi nyumbani na baadaye kuonekana baada
siku tatu akiwa amefia kwenye kisima cha maji.
Kwa
mujibu wa Baba mzazi wa mtoto huyo Maulid Shabani alisema mtoto wake
hakurudi nyumbani siku hiyo waliendelea kumtafuta bila mafanikio na
ndipo baada ya siku tatu walimkuta akiwa amefia ndani ya kisima cha maji
kilicho maeneo ya Kijiji cha Nyankumbu Kitongoji cha Mwembeni.
Baba
huyo alisema baada ya hapo walitoa taarifa Polisi kisha waliruhusiwa
kuuchukua mwili wa mtoto wao na kwenda kuuzika nyumbani kwa kitongoji
cha 14 Kambarage ndani ya mji wa Geita.
Alisema
walifanya shughuli zote za matanga na wakajua tayari mtoto wao
ameishafariki na kwamba hawakuwa na wazo lolote na kumpata siku zote
akiwa hai kama ilivyotokea akisema ni tukio la kustaajabisha kwake.
Mama
mzazi wa mtoto huyo Aziza Ramadhani akisimulia namna alivyokutana na
mtoto wake alisema alikuwa akienda kwenye shughuli zake za ujasiriamali
kama mfanyabiashara ya mbogamboga akiwa amefika eneo la Nyankumbu nje
kidogo sana na mji wa Geita eneo la Mwembeni alikutana uso kwa uso na
mtoto wake.
Alisema
alipomuona alimwita kwa jina lake akisema "mwanagu Shabani ni wewe naye
akamwitikia ni mimi kisha alimshika mkono huku akiwa haamini macho yake
ndipo alipompigia simu mumewe naye akaja wakamchunguza vizuri
wakaabaini kuwa ndiye mtoto wa Shabani aliyesadikiwa kuwa alifariki na
kuzikwa.
Akithibitisha
zaidi mama wa mtoto huyo alisema mwanae alikuwa na alama ya kinundu
kwenye paji la uso na mguuni akiwa na alama ya kovu mguuni
iliyosababishwa na kuchomwa na mwiba pia alikuwa na mwanya uliofanan na
wa baba yake mzazi.
Mtoto
huyo aliyevuta hisia za watu wengi mjini Geita ameendelea
kuthibitishwa na walimu wake wa shule ya Msingi Mwatulole alikokuwa
anasoma darasa la tano kabla ya kifo hicho cha utata kwa sasa.
Akiongea na Mwandishi wa
Makamu mkuu wa shule ya msingi Mwatulole Joseph Nungula aliyekuwa
akifuatilia kwa karibu tukio hilo alisema kweli mtoto huyo anaonekana ni
yeye bila kutia shaka yoyote .
Mwalimu
huyo alisema amemtambua mtoto huyo kwa sura na alama hasa ya usoni huku
akimwelezea mtoto huyo kuwa alikuwa na mahudhurio mazuri shuleni pia
maendeleo yake kitaaluma yalikuwa mazuri.
Mtoto
huyo ambaye anaendelea kupewa huduma ya kitabibu katika Hospitali ya
wilaya ya Geita kwa uchunguzi zaidi wa kiafya anaongea kwa shida
wanapokuwepo watu watu wengi hata hivyo amemtambua Baba na mama yake
mzazi ambapo wanapomuuliza baadhi ya maswali anawajibu.
Jeshi
la Polisi mkoani hapa ambalo lilikuwa likiwa likifuatilia tukio hili
kwa ukaribu sana limethibitisha kutokea kwa tukio hili huku wakiahidi
kuendelea kutoa habari zaidi ambazo tutaendelea kuwajulisha huku
wananchi wakisubiri kibali cha mahakama kufukua kaburi alililokuwa
amezikwa mtoto huyo.
0 comments:
Chapisha Maoni