Searching...
Jumapili, 15 Septemba 2013

KUFURUUUUUU,MKATABA MPYA WA RONALDO WAITIKISA DUNIA.

Ronaldo signs new multi-million pound Madrid contract
CHRISTIANO RONALDO.
Wakati Timu ya Manchester United wakiendeleza mipango butu ya kumrejesha mshambuliaji wao wa zamani mreno Christiano Ronaldo hatimaye mipango yao imegeukakuwa ndoto baada ya timu tajiri duniani yenye utaratibu wa kumwaga mapesa kwa wachezaji bora duniani Real Madrid wamemsainisha Ronaldo mkataba mpya wa miaka mitano mkataba utakaomfanya asiondoke kunako Bernabeu mpaka mwaka 2018. Habari hizi zitatangazwa rasmi na rais wa Madrid Florentino Perez baadae hii leo.
Mkataba huo wa historia katika ulimwengu wa soka utamfanya Ronaldo kuingiza kitita cha paundi milioni 15 kila mwaka baada ya malipo yote ya kodi na hivyo kuingiza paundi milioni 75 katika muda wote wa mkataba wake wa miaka mitano ndani ya klabu hiyo,mkataba ambao ni historia katika sayari hii ya dunia.
Ronaldo signs new multi-million pound Madrid contract
MAJEMBE MAWILI YA MADRID RONALDO NA BALE.
Mktaba huo mpya ni kwaajili ya kumhakikishia Ronaldo kwamba japo Bale amevinja rekodi yake ya kununuliwa ghali lakini bado Ronaldo ni mchezaji bora wa Madrid.
Lakini pia Mkataba huo utaifanya klabu ya Manchester United kuishia kuota ndoto za mchana za kumrejesha Ronaldo kunako ngome kongwe,kwasababu walikua na mategemeo makubwa kwamba angerejea baada ya mkataba wake kumalizika mwaka 2015.

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!