SAMANTHA LEWTHWAITE.
Wakati mapambano bado yanaendelea dhidi
ya wanamgambo wachache wa al Shabaab waliobaki ndani ya Westgate Mall,
maofisa wa Kenya wamesema angalau al Shabaab watatu wameuawa katika
harakati za kuokoa mateka
Taarifa zinasema mmoja wa magaidi hao ni
mwanamke wa kizungu. Inaaminika kuwa mwanamke huyo aliyetajwa ni
Samantha Lewthwaite, al-maarufu kama “White Widow” au “Mjane Mweupe” au
“Mjane wa Kizungu” kwa Kiswahili. Samantha anaripotiwa kuwa ndiye
kiongozi wa kundi hilo lililofanya mashambulizi.
Inasemekana kwamba kati ya magaidi waliouawa, mmoja wao ni mwanamke wa kizungu lakini bado haijajulikana kama ni Samantha.
Kwa mujibu wa gazeti la Daily Mail la
Uingereza, mume wa Samantha alikua mpiga mabomu wa kujitoa mhanga
(suicide bomber) anayeitwa Germaine Lindsay ambaye baada ya kusilimu
alitumia jina la Abdullah Shaheed Jamal.
Abdullah Jamal alikua ni mmoja wa
magaidi wenye asili ya Uingereza waliopiga mabomu ya kujitoa mhanga
katika treni tatu na kuua watu 56 nchini uingereza Julai 7, 2005 ambao
unajulikana duniani kama “Ugaidi wa 7/7″
0 comments:
Chapisha Maoni