Baada ya kukaa barabarani kwa zaidi ya saa tatu leo asubuhi,niliamua kupitia vichochoroni ili kuikacha foleni lakini huwezi amini kila kiuchochoro kilikua kimeziba kama unavyoona.
hiki ni kiuchochoro cha kawe beach ukitokea mbezi beach na hivi ndivyo ilivyokuwa.
baada ya kukwama katika kiuchochoro kimoja nililazimika kutafuta kiuchochoro kingine lakini wapi,kote kulikuwa ni balaa.
nikaamua kugeuza kiubishi ubishi lakini ona picha inayofuata.
ni kama unaruka majivu alafu unakanyaga moto maana huku sasa kulikua hakuna pa kugeuzia.
ukiangalia kwenye kioo cha pembeni hapo kushoto unaona nyomi iliyo nyuma huko,na hapo ni uchochoroni tumenyoosha mikono tunarudi kwenye lami.
angalia na nyomi iliyopo nyuma upande wa kulia.
hapo sio shoo room bali ni barabarani tena bara bara za uchochoroni.
Oooooh,karibia nakaribia kufika kwenye lami,japo ni mwendo wa kinyonga.
jamaa yangu yeye uzalendo umemshinda ameamua kutafuta mahali anywe chai akisubiri miujiza ya kufungua bara bara.
ukiona mpaka piki piki na bajaji hazitembei basi ujue ni balaa.
hatimaye naikanya lami kwa mara nyingine...HII NDIYO DAR ES SALAAM BANAA.
0 comments:
Chapisha Maoni