Searching...
Jumatatu, 16 Septemba 2013

DUNIANI KUNA MAMBO,BAADA YA GARI LAKE KUMSUMBUA KWA MIAKA 4,AAMUA KULICHARANGA MASHOKA HADHARANI.


Huyu jamaa aliyefahamika kwa jina Hadi akiwa na rafiki yake Thomas Brunner wameamua kulisulubu gari la kifahari la kampuni ya BMW M6 kufuatia mmiliki wa gari hilo bwana Hadi kuchoshwa na matatizo ya mara kwa mara ya gari hilo alilolinunua kwa kitita cha paundi laki moja mwaka 2008.
Bwana Hadi ambaye anaishi nchini Italia anasema gari hilo limemsumbua kwa takribani miaka minne ambapo amesema amelipeleka kwenye gereji nyingi za BMW bila mafanikio.
akizungumza na gazeti moja la Ujerumani bwana Hadi ameongeza kuwa BMW ya Italia na makao makuu ya Munich hawajamsaidia lolote katika kutatua matatizo ya gari lake kwani amewaandikia barua mara kwa mara pasipo majibu na ndio akaona njia pekee ya kuonyesha kama amechoka ni kufanya alichokifanya.
Mzungumzaji wa kampuni ya BMW amesema kampuni itahusika na kesi hiyo ya bwana Hadi.

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!