Searching...
Alhamisi, 29 Agosti 2013

YANGA HAIPENDI KUFUNGWA-WASHAMBULIA GARI LA COSTAL,MCHEZAJI APASULIWA KICHWA ASHONWA

Mbali ya mwamuzi kufanya kisichotarajiwa kwa timu zote mbili lakini mashabiki wa Yanga bado walishikilia kuwa Coastal Union wamebebwa hata kuzawadiwa penalt dakika ya 90 na nahodha Jerry Santo kutumbukiza wavuni na kugeuza matokeo kuwa 1-1. Hata hivyo gari la wachezaji wa Coastal Union lilishambuliwa na mashabiki wa Yanga hata kuvunjwa kioo cha pembeni na beki wa Coastal Union Hamad Juma kupasuliwa sehemu ya kichwa akashonwa nyuzi kadhaa. Viongozi wa Coastal Union wanauliza je huu ni uungwana?

0 comments:

Chapisha Maoni

:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Back to top!