Mkurugenzi
wa Fedha na Utawala wa TMAA Bruno Mteta, akizungumza na waandishi wa
habari
jijini Dar es Salaam kuhusu madini yaliyokamatwa.
wa pili kushoto
ni Ofisa habari wa TMAA,
Mhandisi, Yisambi Shiwa na kulia ni Mkurugenzi
wa Uthaminishaji Madini na Huduma za Maabara,
Mhandisi, Rwekaza
Dominic.
Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa TMAA
Bruno Mteta, akifafanua jambo. Kushoto ni Ofisa
habari wa TMAA, Mhandisi, Yisambi Shiwa.
Bruno Mteta, akionesha sehemu ya madini
yaliyokamatwa.
Sasa tumeanza kazi.
Haya ni baadhi ya madini yaliyokamatwa na TMAA.
Na Irene Mark
WAKALA wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) umekamata
shehena ya madini yenye thamani ya zaidi ya sh bilioni 13 katika kipindi cha
miezi 10 iliyokuwa ikitoroshwa nchini kinyume cha utaratibu.Madini hayo yalikamatwa kwenye viwanja mbalimbali vya ndege
hapa nchini ambapo wakaguzi wa TMAA kwa kushirikiana na Idara ya Uhamiaji,
Usalama wa Taifa, watumishi wa Mamlaka ya Mapato (TRA), Jeshi la Polisi na
wafanyakazi wa viwanja vya ndege (TAA).
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ofisi za wakala
huyo jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa TMAA Bruno
Mteta alisema madini hayo yalikamatwa kati ya Septemba mwaka 2012 na Julai
mwaka huu katika matukio 23 tofauti.
Alisema kwa mwezi huu tayari wakala huyo umewakamata raia
wawili wa kigeni wakiwa na shehena ya madini wakitaka kutoroka nayo huku
akisisitiza kwamba watapandishwa kizimbani wakati wowote.
“Agosti 20 mwaka huu tumewakamata raia wawili wa kigeni
mmoja alikuwa anasafiri amekamatiwa uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu
Nyerere (JNIA) akiwa na madini ya vito yenye thamani ya sh milioni 25.32.
“…Wa pili amekamatwa akiwa kwenye makazi yake Jangwani
Beach hapa jijini kwa kweli thamani ya madini ya mtuhumiwa huyu
hayakutambukuka,” alisema na kuongeza kuwa serikali imeyataifisha madini hayo.
Kwa mujibu wa Mteta wafanyabiashara wa kigeni na wazawa
wanaruhusiwa kusafirisha madini hayo kwa kuzingatia utaratibu ili serikali
ipate mgao wake huku akisisitiza kwamba serikali inategemea mapato ya madini
kujiendesha.
Awali mkurugenzi huyo alisema tangu mwaka 2009 hadi
mwishoni mwa mwaka jana serikali imepokea sh bilioni 317.74 ambazo ni mrabaha
uliolipwa na kampuni 10 kubwa za madini hapa nchni.
Alisema hivi sasa wizi wa madini kwenye migodi mikubwa
haupo kutokana na uwepo wa watumishi wa TMAA wanaotoa ripoti ya uzalishaji kila
siku na kwamba wafanyabiashara wa madini wanaoongoza kwa kukwepa kodi ni
wazawa.
Mteta alieleza changamoto zinazoukabiliwa wakala huyo kuwa
ni kushindwa kuifikia mipaka yote inayounganisha nchi jirani (njia za panya)
ambazo hutumika na wafanyabiashara wengi kutorosha madini hayo.
Alisema watoroshaji wengi wa madini hayo ni wageni kutoka
nchi mbalimbali ambao wanauziwa madini na watanzania na kufafanua kwamba kati
ya matukio 23 watanzania wawili.
Mkurugenzi huyo alisema tayari kesi tatu kati ya 23
zimesikilizwa na kutolewa hukumu na kutoa mfano wa kesi ya mgeni aliyekamatwa
na madini yenye thamani ya zaidi ya Dola 6,200 za Marekani alitozwa faini ya sh
milioni 1.5 na madini yake kutaifishwa na serikali.
0 comments:
Chapisha Maoni