Pichani juu ni sehemu washiriki wa semina ya Fursa kwa vijana, wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikizungumzwa kwenye semina hiyo, ambayo imeonekana kuwavutia vilivyo kwa sehemu ya wakazi wa mji wa Singida waliojitokeza kushiriki.…
Pichani juu ni sehemu washiriki wa semina ya Fursa kwa vijana, wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikizungumzwa kwenye semina hiyo, ambayo imeonekana kuwavutia vilivyo kwa sehemu ya wakazi wa mji wa Singida waliojitokeza kushiriki.
Mwakilishi
wa Shiriki la NSSF kutoka Makao Makuu jijini Dar,Bwa.Salim Khalfan
akielezea fursa mbalimbali zinazopatikana kwa mtu yeyote anayejiunga na
shirika la NSSF,alifafanua hayo leo kwenye ukumbi wa Luluma,nje kidogo
ya mji wa Singida, Salim alibanisha kuwa mtu yeyote atakayejiunga na
shirika hilo atanufaika na mambo mengi,ikiwemo suala la matibabu, mikopo
na mengineyo lukuki yanayopatikana ndani ya shirika hilo. Semina hiyo
ambayo inafanyika ikiwa ni mkoa wa tatu huu, ikianzia Kigoma,Tabora na
sasa Singida,iliandaliwa na Clouds Media Group na kufadhiriwa na shirika
la NSSF, Zantel, MaxMalipo, Lake Oil.
Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji kutoka Clouds Media Group,Ruge
Mutahaba,akizungumza mbele ya washiriki wa Semina ya Fursa ndani ya
ukumbi wa Luluma,nje kidogo ya mji wa Singida, kuhusiana na fursa
mbalimbali wanazozipata vijana na kuhakikisha wanazitumia
ipasavyo,aliongeza kuwa vijana wengi wamekuwa ni watu wa kulalamika
lalamika tu na kukata tamaa mapema,aidha Ruge amewataka vijana kuwa na
muamko wa kufanya kazi na kujituma kwa bidii pale fursa yoyote
inapotokea.
Mmoja
wa Watangazaji mahiri wa Clouds FM, Millard Ayo akizungumza mbele ya
vijana wenzake, namna alivyobahatika kuzitumia fursa mbalimbali
alizokuwa akizipata kwa ufasaha na kwa umakini mkubwa mpaka hapo
alipo,anabainisha kuwa kilichompelekea hapo alipo mpaka sasa ni namna
alivyojijenga kwa nidhamu,kujituma na bidii kubwa ya kazi kila alipokuwa
akiipata fursa,aidha amewataka vijana wenzake kuacha tabia ya kukata
tamaa mapema na kutokuwa wavivu wa kufanya kazi,kwani kwa kufanya hivyo
maendeleo hayatapatikana kirahisi.
0 comments:
Chapisha Maoni