Searching...
Jumamosi, 24 Agosti 2013

MTOKO WAZUA MAJANGA,GARI YAPONDWA JIWE,POMBE ZOTE ZAISHA KICHWANI

 Jamaa mmoja ambaye alikuwa amejitwika pombe za kutosha alijikuta katika hali ngumu baada ya kugeuza gari yake aina ya toyota 110 na kugonga gari ya mtu mara tatu huku akiwa amefunga vioo,kila akiambiwa unagonga gari la watu yeye akawa hajali,basi mwenye gari inayogongwa akachukua jiwe kubwa na kuitwa gari ya mlevi kwenye kioo cha nyuma kama unavyoona.
 Tukio hili la aina yake lilitokea sinza Mori kwenye bar ya EGO usiku wa ijumaa kudamkia jumamosi majira ya saa nne usiku.
 Baada ya tukio hilo jamaa alishuka kwenye gari na kushindwa kuamini kilichotokea huku pombe zote kichwani zikionekana kumtoka
 Namba za gari iliyotwangwa jiwe
Muda mfupi baada ya kutwangwa jiwe..jamaa aliyelitwanga hili gari jiwe aliondoka muda huo huo na kuwaacha watu wakiwa wameduwaa wasijue la kufanya.

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!