Searching...
Jumatatu, 5 Agosti 2013

MASHINDANO YA KUSOMA NA KUHIFADHI QURANI MKOA WA MBEYA

Mtoto Habibu Abdulrahman(8) ambaye amehifadhi juzuu ya kwanza akionesha umahiri wake wa kuhifadhi na kusoma Koran katika mashindano yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Tausi Hotel ya Rift Valley Jijini Mbeya jana mchana, Abdulrahman amekuwa mshindi wa kwanza kwa kusoma na kuhifadhi koran juzuu moja
Mtoto Abubakar Muharram(12) akionesha umahiri wa kusoma Koran na kuhifadhi Juzuu saba wakati wa mashindano ya yaliyofanyika Ukumbi wa Tausi Hotel ya Rift Valley Jijini Mbeya, Abubakar amekuwa mshindi wa kwanza katika kundi la wanafunzi waliojitokeza kusoma na kuhifadhi Juzuu Saba amepewa zawadi ya Msahafu maalum unaotumia umeme na fedha taslimu Sh.80,000
Majaji wakifuatilia kwa makini mashindano ya kusoma Koran kabla ya kupatikana washindi
Mgeni rasmi Shekh Said Jabir pamoja na baadhi ya maimamu wakifuatilia mashindano hayo
Majaji wakiwa kazini kumtafuta mshindi
Mgeni rasmi Shekhe Said Jabirakitoa nasaha kabla ya kupatikana kwa mshindi
Mgeni rasmi akimpa mkono mmoja wa majaji wa mashindano hayo Shekhe Abbas Mshauri
Mgeni rasmi akimpongeza mshindi wa kwanza wa kusoma na kuhifadhi Koran na Juzuu moja

Mshereheshaji wa mashindano hayo Shekhe Ibrahimu Bombo akiwaongoza wasomaji na wahifadhi wa Koran
Mshindi wa kwanza wa kusoma Koran juzuu saba Abubakar Muharam akiwa na msahafu wake wa Digital
 Baadhi ya waumini na wanafunzi wa madrasa mbalimbali waliohudhuria mashindano ya kusoma Koran
Picha zote na  Rashid Mkwinda

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!