Helikopta maalum
iliyowabeba viongozi wa CHADEMA akiwemo Mwenyekiti wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Mbunge wa Jimbo la Hai, Mh. Freeman
Mbowe pamoja na Mbunge wa jimbo la Ubungo Mh. John Mnyika walipowasili
eneo la Mnada Wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza kufanya mkutano wa
hadhara wilayani humo mwishoni mwa Juma.
Mwenyekiti wa Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Mbunge wa Jimbo la Hai, Mh.
Freeman Mbowe akihutubia wakazi wa wilaya ya Sengerema Mkoa wa Mwanza
mwishoni mwa juma kwenye mkutano wa hadhara. (Picha na Zainul Mzige wa
Mo Blog).
Mwananchi wa Geita ambaye jina lake halikuweza kupatikana kiurahisi akitoa maoni yake ya Rasimu ya Katiba Mpya mbele
umati wa wafuasi wa Chadema na wakazi wa wilaya hiyo ambapo wengi wao
wametaka Ushuru wa Masoko ufutwe pamoja na baadhi ya kinamama
kulalamikia shida ya Maji kwenye Wilaya hiyo na Mh.Mbowe aliwaasa kutumia Mabaraza ya CHADEMA kuwasilisha maoni yao wakati wa mkutano wa hadhara.
Mbunge wa Jimbo la
Ubungo Mh. John Mnyika akiteta jambo na mmoja wa viongozi wa Chadema
wilayani Sengerema Hemedi Sabula wakati wa mkutano huo wa hadhara.
Na. Mwandishi wetu.
Mwenyekiti wa Chama
cha Domokrasia na maendeleo (CHADEMA) Mh.FREEMAN MBOWE amewataka
Watanzania kujitokeza kwa wingi kujadili Rasimu ya Katiba mpya ili
ipatikane Katiba itakayokidhi haja ya Watanzania.
Amesema hayo
alipokuwa akiwahutubia wakazi wa wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza
alipokuwa kwenye ziara ya kichama kuhamasisha wanachama wa chama hicho
kuunga mkono kuwepo na Serikali tatu ndani ya Jumuiya ya Muungano wa
Tanzania.
Amesema kuwepo
Serikali tatu siyo mzigo kama Chama cha Mapinduzi (ccm) kinavyosema ila
tunataka kuwepo serikali ya Tanganyika na Zanzibari na ile ya muungano
ili kuleta usawa ndani ya Muungano huo.
Pia amesema kuwa
Lugha ya Kiingereza na Kiswahili ipatiwe kipaumbele kufundishwa kuanzia
daraja la awali hadi Chuo Kikuu ili kuwajengea Watanzania kufahamu Lugha
ya Kiingereza vema na kupata ajira kwa urahisi.
0 comments:
Chapisha Maoni