Searching...
Alhamisi, 8 Agosti 2013

FABREGAS AVUNJA UKIMYA ACHOMOZA KWENYE VYOMBO VYA HABARI ASEMA SIONDOKI BARCA

Fabregas rules out Manchester United transferCESC FABREGAS AKIFURAHIA JAMBO NA WACHEZAJI WENZAKE WA BARCELONA.
Hatimaye mchezaji wa kimataifa wa Hispania na klabu ya Barcelona Cesc Fabregas ameamua kujitokeza hadharani na kuvunja ukimya uliotawala kwa muda mrefu kuhusiana na kuhusishwa na taarifa za kutakiwa na klabu ya Manchester United ya England na kusema yeye maisha yake yapo Barcelona.
Nahodha huyo wa zamani wa Arsenal alihusishwa na taarifa za kutua Old Trafford baada ya Manchester United kutuma ofa mara mbili na kugonga mwamba na sasa wakiwa wanajiandaa kutuma ofa ya tatu.
Hata hivyo Fabregas amewashukuru United kwa kuonyesha kwamba yeye ni mchezaji bora lakini amesisitiza kwamba asilimia 100 ya ndoto za maisha yake zipo Barcelona.
‘Nimekua kimya kwa muda mrefu sasa,na ninajua watu wengi wanataka niweke mambo wazi kuhusu tetesi zilizopo kati yangu,Barcelona na Manchester United,Tangu nikiwa mtoto nilikua na ndoto za kuwa Barcelona,’alisema Fabregas.
FC Barcelona's Neymar (L) congratulates his teammate Cesc Fabregas (L) after he scored during their exhibition match Barcelona vs Thailand at the rajamangala football stadium in Bangkok on August 7, 2013. Barcelona won 7-1 against Thailand. AFP PHOTO/ Nicolas ASFOURINICOLAS ASFOURI/AFP/Getty Images
CESC FABREGAS AKIPONGEZANA NA MCHEZAJI MWENZAKE NEYMAR
‘Ndoto zangu hazijabadilika,ni kweli kwamba ushindani wa namba hapa klabuni ni mkubwa,lakini nimekuwa nikijitahidi kufanya vizuri siku hadi siku
‘Ni heshima kubwa sana kupewa ofa mara mbili na manchester United, lakini hakukuwa na mazungumzo yoyote kuhusu hili,sijawahi kuongea na timu yoyote kuhusu uhamisho tangu nijiunge na Barça miaka miwili iliyopita.
‘Mara zote nimekuwa nikithaminiwa sana na timu yangu,kila mtu amekua akiniambia wananitegemea,sijawahi kuwa na dalili zozote za kufikiria tofauti na hivyo.
‘sina haja ya kusahihisha chochote,kwasababu kwangu ni dhahiri ninataka kusalia klabuni hapa,nimewaambia viongozi wangu hivyo.’Fabregas alifunguka namna hiyo.

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!