Kocha mkuu wa Tottenham Andre Villas-Boas ametoboa siri kwamba mchezaji wake anayewaniwa na matajiri wa Hispania klabu ya Real Madrid Gareth Bale haongei naye kabisa kama moja ya njia ya kushinikiza kuondoka kwake klabuni hapo na kutimkia kunako Real Madrid.
Madrid wamemuweka Bale kama mchezaji wao namba moja katika kipindi hiki cha uhamisho japo tayari wameshakwama mara mbili pamoja na kupeleka ofa nono ya kihistoria ya paundi milioni 85.
Kwa upande wao Spurs wameendelea kusisitiza kwamba mchezaji wao hauzwi lakini sasa kwa mujibu wa kocha wa spurs Villas-Boas kwamba Bale amesusa kuongea naye tayari ni neema kwa Madrid
‘Huyu ni mchezaji wetu,mipango yetu ni kumjumuisha kwenye kikosi chetu msimu huu...
‘Tunajua Real Madrid wanapambana usiku na mchana kumsajili,haimaanishi kwamba tupo tayari kufanya nao mazungumzo...
‘Ana matatizo ya akili? hakuna anayejua kwasababu hataki kuzungumza‘alisema AVB
‘Kitu pekee tunachokitaka kwake ni kumuona anakuja mazoezini,anafanya mazoezi na kuondoka’aliongeza Villas-Boas.
Tetesi hizo za kuvunjika mahusiano ya kimawasiliano kati ya Bale na Villas-Boas zilianza kusikika pale tu mchezaji huyo alipoonyesha nia ya kujiunga na Madrid.
Kwa mujibu wa gazeti moja la Hispania taarifa zinasema tayari Bale ameshawaambia marafiki zake na familia yake kwamba anataka kujiunga na Carlo Ancelotti na taarifa zaidi kutoka Madrid
zinasema kwa sasa wapo kwenye maandalizi ya kupeleka ofa nyingine kwa Tottenham ambayo wanaamini watamuachia mfumania nyavu huyo kutua kunako Bernabeu.
Ofa hiyo inatarajiwa kuwa ya paundi milioni 90 ambayo italipwa kwa vipindi viwili ambapo pia watamtoa na mchezaji wao Fabio Coentrao kama kilainishi cha dili hilo
0 comments:
Chapisha Maoni