hospitali ya Kamango imeporwa na wagonjwa wote walipigwa fimbo na waasi wa ADF wakiungana na Mai Mai wengi wao wakiwa ni watoto wadogo walioonekana karibu na Kamango.
jeshi la Congo FARDC ladhibiti kamango na Nobili mpakani mwa Congo na Uganda huyu ni Meja KAKULE BUTALA aliyekomboa maeneo hayo tangu jana ijumaa tarehe 12/07/2013 akiwa na askari wake katika kambi ya kijeshi pa Nobili kupitia uongozi wa Kanali Bisamaza.
Huu ni mwili wa kiongozi wa asili aliye uliwa na waasi waADF NALU katika kijiji cha kamango Drc jana ijumaa july 12,2013

Huyu mama amepoteza watoto sita kaka yake na mumewe hadi sasa haijajulikana kama wameuwawa au wametekwa.
Hao ni wanajeshi wa Uganda wakilinda mipaka ya nchi yao na wamesema hawataingia DRC ila watahakikisha waasi hao hawaingii Uganda





0 comments:
Chapisha Maoni