Klabu ya Valencia ya Hispania imetangaza dau nono la kumtaka Fernando Torres ili kuziba pengo la Roberto Soldado ambaye ameonyesha kila dalili ya kutua Tottenham kwa kitita cha paundi milioni 25.8.
Bosi wa Valencia Miroslav Duckic ameamua kuelekeza juhudi zake kwa Torres baada ya kujaribu bila mafanikio kumnasa mshambuliaji wa Arsenal Olivier Giroud, na vile vile juhudi za kumnasa mshambuliaji wa Real Zaragoza mreno Helder Postiga kugonga mwamba.
Valencia wanaonekana wanaweza wakabahatika kumnasa Torres kiurahisi sana baada ya uwezekano wa Chelsea kumnasa Wayne Rooney na hivyo kuonekana hana nafasi ten,Fernando Torres amekuwa katika wakati mgumu Chelsea tangu atue akokea Liverpool kwa kitita kilichovunja rekodi cha paundi milioni 50 mwaka 2011
0 comments:
Chapisha Maoni