DEMA BA AKIWA KAZINI CHELSEA.
Hatimaye katika kile kinachoonekana kama msimamo wa kocha mpya wa chelsea mreno Jose Mourinho kukiimarisha kikosi chake kwa kuuza wachezaji asiowahitaji na kunuua wengine mshambuliaji Demba Ba ameonekana akifanya mazungumzo na klabu ya Anzhi Makhachkala.
taarifa zinasema mshambuaji huyo atafuatiwa na kiungo John Obi Mikel baada ya klabu hiyo kufanikiwa kumpata kiungo Marco van Ginkel, Ba alikataa kurejea West Ham United, klabu ambayo alishawahi kuichezea na alitarajiwa kusaini West Bromwich Albion,lakini klabu hiyo tayari imeshaingia mkataba na mshambuliaji wa zamani wa Chelsea Nicolas Anelka.
GONZALO HIGUAN
Mshambuliaji wa Real Madrid na timu ya taifa ya Argentina Gonzalo Higuaín amekamilisha dili lake la uhamisho kwenda Arsenal kukipiga msimu ujao kwa kitita cha uhamisho wa paundi milioni 2.
usiku wa kuamkia hii leo Arsenal walikua katika hatua za mwisho mwisho kumalizana na Gonzalo Higuaín dili litakalomfanya muajentina huyo kuwa mchezaji ghali zaidi na mchezaji anayelipwa fedha nyingi kuliko mwingine yoyote ndani ya klabu hiyo ya Arsenal.
WAYNE ROONEY.
Ile sinema ya Wayne Rooney inaendelea ambapo sasa luninga inaonyesha sterling namba mbili wa sinema hiyo ambaye pia ndiye kocha mkuu wa man u David Moyes pamoja na mkurugenzi mkuu wa Man U Ed Woodward wamefanya mazungumzo na Sterling mwenyewe Rooney pamoja na wakala wake Paul Stretford na kukubali kwamba katika kikao walichofanya Rooney na Mzee Ferguson mwezi wa nne mwaka jana mchezaji huyo hakumuambia kocha huyo kwamba anataka kuondoka klabuni hapo kwahiyo inamaanisha kwamba Babu Ferguson ni muongo alimsingizia Rooney.
Man United
bado wameshikilia kauli yao kwamba Rooney hauzwi na bado anao mkataba na klabu hoyo wa miaka miwili kuanzia sasa
Kwasababu hiyo David Moyes anatarajiwa leo kukutana na vyombo vya habari kutangaza rasmi kwamba Rooney ataendelea kukipiga na klabu hiyo msimu ujao kauli ambayo itakuwa mwiba mchungu kwa Chelsea,Arsenal na Real Madrid ambao walikuwa wakimmezea mate kila kukicha
lakini jeee,Rooney Mwenyewe amekubalii?
sinema hii itaendelea kesho hapa hapa
MCHOME BLOG USIKOSEEEEE.
Newcastle United wapo katika harakati za kumsajili Arouna Kone.
Wigan wametoa ruksa kwa United kuzungumza na nyota huyo wa Ivory Coast.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 anauzwa kwa kitita cha paundi milioni 5 japo Everton walionyesha nia kubwa ya kumsajili nyota huyo lakini
Newcastle United wanaamini watamnyakua mchezaji huyo.
HULK.
Mbrazili huyo mwenye miaka 26 amekuwa akifuatiliwa kwa karibu sana na mreno Jose Mourinho ambapo taarifa za uhakika zinasema tajiri na mmiliki wa klabu ya Chelsea Roman Abrahimovich amempa ruhusa pamoja na kitita cha paundi milioni 40 ili kuipata huduma ya mchezaji huyo
Wakati huo huo timu ya Tottenham inayonolewa na mreno pia nao wapo tayari kumnunua mchezaji huyo ambapo katika hali inayoonekana itawavutia zaidi Besiktas tayari Spurs wamepokea ofa kutoa kwao ya kumtaka Emmanue Aderbayo kwa ada ya shilingi milioni 6 hali ambayo inweza ikawa rahisi kubadilishana wachezaji hao na Spur kuongeza fedha
LUIS SUAREZ
Klabu ya Liverpool imemtaka mchezaji wao ambaye amekuwa haeleweki msimamo wake Luis Suarez kumaliza swaga za uhamisho wake na hatma yake kabla mwisho wa mwezi huu.
0 comments:
Chapisha Maoni