Searching...
Jumanne, 9 Julai 2013

RONALDO KUMALIZIA SOKA MADRID,ARSENAL HAWAJATUMA OFA KWA HIGUAN,MOURINHO KUHAMISIHIA NGUVU KWA SUAREZ

Staying: Speaking at an event in Monaco, Cristiano Ronaldo said his future lies at Real Madrid

CHRISTIAN RONALDO.
Rais wa klabu ya Real Madrid Florentino Perez.amekaririwa na vyombo vya habari akisema mchezaji wake Cristiano Ronaldo atamalizia soka lake Madrid
mshambuliaji huyo wa ureno mwenye umri wa miaka 28, siku za hivi karibuni amehusishwa na kuhamia kwenye klabu yake ya zamani ya Manchester United au Monaco lakini Perez amesema ni hakika Christian Ronaldo atamalizia soka lake akiwa na miamba hiyo ya soka ya Hispania.
Real Madrid and Argentina striker Gonzalo Higuaín close to confirming £22 million move to Arsenal
GONZALO HIGUAN.
Akaongeza kwamba Madrid hawajafanya mazungumzo yoyote ya maafikiano ya kumnunua mchezaji wa Tottenham Gareth Bale wala kupokea ofa yoyote kutoka kwa Arsenal ya kumtaka  Gonzalo Higuain zaidi ya kusikia habari hizo kupitia vyombo vya habari 
LUIS SUAREZ.
Kocha wa Chelsea Jose Mourinho yupo tayari kutoa kitita cha paundi milioni 40 kwaajili ya kuinasa saini ya mshambuliaji wa Liverpool striker Luis Suarez ambaye hana mpango wa kuendelea kukipiga na majogoo hao wa anfield msimu ujao.
Jose Mourinho akijua atakutana na upinzani mkubwa kutoka Liverpool kama ilivyotokea kwa Arsenal kukataliwa ofa yao ya kumtaka mchezaji huyo 
Suarez anacho kifungu cha sheria katika mkataba wake kinachowalazimisha Liverpool kumuuza wakati wowote akitaka kwa kitita kisichopungua paundi milioni 40 lakini wao wanasema hawawezi kumuuza kwa kiasi hicho kidogo kulingana na thamani yake.
Mmiliki wa klabu ya Chelsea tajiri wa Kirusi Roman Abramovich yupo tayari kumpa Mourinho kiasi chochote cha pesa kwaajili ya kumpata mshambuliaji bora duniani ambapo baada ya malengo yao ya kuwanyakua Hulk, Radamel Falcao na Edinson Cavani kushindikana sasa wanaelekeza nguvu zao kwa  Suarez.

Highly rated: David Luiz is among the best defenders in the Premier League
DAVID LUIZ
Klabu ya Barcelona imetuma ofa ya paundi milioni  30 kwaajili ya kumnasa beki nguli mbrazili David Luiz lakini Chelsea hawataki kumuuza mchezaji huyo kwa kiasi hicho kidogo cha fedha.


0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!