ODOM LAMAR AKIPAMBANA NA MPIGA PICHA.
Odom Lamar mwenye urefu wa futi 6 mchezaji nyota wa mpira wa kikapu maarufu kama basketball ameleta sokomoko kubwa nchini Marekani jana baada ya kumtwanga makondo mazito mpiga picha aliyekuwa akimpiga picha barabarani bila idhini yake
Lamar, mchezaji maarufu nchini marekani mumewe na Khloe Kardashian, ambaye siku zote anafurahia kupigwa picha lakini jana alionekana kutokuwa sawa au kutokuwa na mood
"weka kamera yako chini tuongee mimi na wewe ana kwa ana"aling'aka namna hiyo Lamar... lakini mpiga picha hakutaka kuweka kamera yake chini na kuendelea kumpiga picha ndipo sokomoko likaanza...
Lamar aliufungua mlango wa gari la mpiga picha na kuchukua chuma moja na kuanza kumshikisha adabu mpiga picha huyo kama anavyoonekana pichani hapo juu.
Hapa mpiga picha akimsihi Lamar kuweka chuma chini lakini akaenda kwenye gari la mpiga picha mwingine na kufungua mlango na kuanza kulibonda bonda gari hilo kisha akaenda kwa mpiga picha mwingine na kufungua mlango wa gari lake na kuchukua begi kubwa la kamera na kulifungua kisha akamwaga vitu vyote vilivyokuwemo ndani na kusambaa barabarani.
Hapa mbabe Lamar akiwa amebeba begi kubwa la kamera huku akiwa ameshikilia chuma aliyoitumia kufanya fujo akielekekea kwenye gari lake.
Hili lilikua ni tukio la kusisimua sana hadi madereva na watalii walilazimika kusimama au kupunguza mwendo na kushuhudia tukio huku wakipiga picha na baada ya kumaliza vurugu zake aliingia kwenye gari lake la kifahari aina ya Mercedes na kutokomea na kuwaacha wapiga picha wakiwa wameshikwa na butwaa wasijue la kufanya.
0 comments:
Chapisha Maoni