Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania,
Generali Devis Mwamunyange akifungua rasmi Mkutano wa Makatibu Wakuu na
Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na
Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC)
uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere
Jijini Dar es Salaam tarehe 10 Julai, 2013. Mkutano huo ni maandalizi
ya mkutano wa Mawaziri wa Asasi hiyo utakaofanyika tarehe 13 Julai,
2013.
Baadhi ya Wajumbe kutoka nchi
wanachama wa SADC wakimsikiliza Generali Mwamunyange (hayupo pichani)
wakati wa ufunguzi wa mkutano huo.
Wajumbe wengine wakati wa mkutano huo.
Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa masuala
ya Usalama nchini Namibia, Bw. Ben Likando na Bw. Tom Moyane, Kamishina
wa Magereza wa Afrika Kusini wakati wa ufunguzi wa mkutano wa asasi
hiyo. Tanzania ni Mweneyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya
SADC wakati Namibia ni Makamu Mwenyekiti wa Asasi hiyo na Afrika
Kusini ilikuwa Mwenyekiti kabla ya Tanzania.Picha na Wizara ya Mambo ya nje na ushirikiano wa Kimataifa
0 comments:
Chapisha Maoni