
Baada Waziri wa Ujenzi, Pombe Magufuli kutoa maagizo kwa wenye majengo
yaliyo pembezoni mwa barabara ya Ali Hassan Mwinyi, kubomoa wenyewe
majengo yao ili kupisha upanuzi wa barabara hiyo, kuonekana yakisua sua,
hatimaye leo ameanza rasmi kazi ya kubomoa kwa Greda katika majengo ya
wale walioonekana kukaidi agizo hilo.
Katika kutekeleza agizo hilo zoezi hilo limeanzia kwenye Jengo la Business Park (Green Acres) lililopo eneo la Victoria ambapo hadi hivi sasa zoezi hilo bado linaendelea pande hizo chini ya usimamizi ya Askari
Katika kutekeleza agizo hilo zoezi hilo limeanzia kwenye Jengo la Business Park (Green Acres) lililopo eneo la Victoria ambapo hadi hivi sasa zoezi hilo bado linaendelea pande hizo chini ya usimamizi ya Askari
Msongamano pande hizo.....
Tayari ukuta ukiwa umeshashushwa chini wa upande wa barabarani huku baadhi ya watu wanaofanya shughuli zao katika jengo hilo wakihaha kuhamisha baadhi ya vifaa.
Wakati likianza zoezi hilo ndani walikuwapo watu wanaoendesha shughuli zao katika jengo hilo.
Baadhi ya wanaofanya shughuli zao katika jengo hilo wakiduaa wasijue la kufanya.......
Umeshashushwa upande mmoja.
Huu ni upande wapili wa jengo hilo.
Ni upande wa mbele wa jengo hilo zima unavyoonekana....
Jamaa wakisimamia usalama pande hizo wakiwafukuza raia waliokuwa wamekusanyika eneo hilo na kuongoza magari kuondoa foleni eneo hilo.....
Katapila likifanya yake
(Picha zote kwa hisani ya jamii Forum)
0 comments:
Chapisha Maoni