Meno
hayo ya tembo kwa mahesabu ya kawaida ni sawa na Tembo 35 ndiyo wameuawa na
kwamba thamani ya meno hayo ni zaidi ya sh, milioni 850 fedha za
kitanzania.
Akithibitisha
tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoani Pwani Ulrich Matei amesema watuhumiwa hao
wamekamatwa saa 5.30 usiku wa Julai 28 huko Kisarawe na Askari Polisi na
maliasili wilayani humo waliokuwa kwenye operesheni ya kukamata pembe za ndovu.
Matei
amesema watuhumiwa hao walikamatwa katika kizuizi cha Kauzen kata ya Vikumbulu
tarafa ya Chole ambapo walikuwa wakisafirisha meno hayo kwa kutumia gari T 357
ABK Toyota Surf kutoka wilayani humo kwenda jijini Dar esalaam
Kamanda
huyo wa Polisi Pwani amewataja watuhumiwa hao ni Hamidu Hamadi wa Tandika
Yombo, Musa Muhamed Ali wa Kinondoni Studio, Prospa Maleto mkazi wa Tandika
hewa, Amir Bakar mkazi wa Mbagala Chalambe,Seif Mdumuka, Said Kadro na Ramadhan
Athumani wa Chanika.
Matei
amewataja pia askari Polisi wawili waliokamatwa pia kuwa ni Koplo Senga
Idd Nyembo na PC Issa Mtama ambao wote wanadaiwa ni watumishi wa Jeshi la
Polisi kituo cha Ostabay jijini Dar esalaam na wanatarajiwa kutolewa
Kisarawe walikokamatiwa na kufikishwa Kibaha makao makuu wa jeshi hilo mkoani
Pwani kwa ajili ya hatua zingine za kisheria ikiwemo kufikishwa mahakamani.
Chanzo:
tabianchi
0 comments:
Chapisha Maoni