Mwandishi wa habari wa ITV na Radio One nchini DRC Austere Malivika akiwa na Brigedia Generali Mwakibolwa wa majeshi ya umoja wa mataifa wanaolinda amani nchini DRC ofisini kwake Goma leo asubuhi.Kamanda huyo
wa kikosi cha UN kutoka Tanzania Brigedia generali MWAKIBOLWA amesema
kuwa hakuna hata kundi moja la waasi litakalo ingia Goma huko Drc hata
iwe usiku, nakuwa M23 ikiwa inania hiyo nikupoteza muda wake.
Brigedia
Generali MWAKIBOLWA kamanda wa kikosi cha UN kitakachoshughulikia
waasi asema kuwa hakuna askari wa Tanzania aliyetekwa na waasi wa M23 bali M23
imeonekana kuwa na nguvu katika propaganda ili kuwatisha askari waliopo nchini humo.
waandishi habari wakiwa katika mkutano na viongozi wa umoja wa mataifa Goma nchini DRC.
Askari moja wa FARDC na polisi wamefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kuzalilisha maiti kunako uwanja wa mapigano kaskazini mwa Mji wa Goma huko Kivu kaskazini.askari huyu na polisi wasema kuwa watasubiri mawakili wao ili wajitetetee vilivyo mbele ya vyombo vya sheria.
Kiongozi wa umoja wa mataifa huko Goma nchini DRC akizungumza na waandishi wa habari hii leo kuhusiana na haki ya mwanamke pamoja na majukumu yao.
Wanawake huko Goma wakimsikiliza kiongozi wa UN Kivu kaskazini kunako jengo la akina mama Mjini humo.
HABARI NA PICHA NA AUSTERE MALIVIKA DRC
0 comments:
Chapisha Maoni