JOHN MNYIKA-MBUNGE WA UBUNGO
July 25, 2013 at 2:37pm
Leo
tarehe 25 Julai 2013 chombo kimoja cha habari kimemnukuu Mwenyekiti wa
Kamati ya Bajeti Andrew Chenge (Mb) akisema kwamba uamuzi kuhusu
kodi/tozo ya kadi/laini za simu haukuwa wa kubahatisha. Chenge amesema
kwamba kamati yake ilifanya utafiti wa kina na kisha kufikia uamuzi wa
kuona tozo hiyo ni sahihi.
Ni muhimu akatakiwa kupitia
namba yake 0754782577 atoe maelezo zaidi kuhusu usahihi wa tozo hiyo na
aeleze ni wapi wananchi na wadau mbalimbali wanaweza kupata vielelezo
vya utafiti walioufanya.
Aidha, wenye maswali kuhusu nini
hasa kilijiri kwenye kamati ya bajeti mpaka kamati hiyo ikakataa jedwali
la marekebisho nililoliwasilisha tarehe 27 Juni 2013 kabla ya muswada wa
sheria ya fedha kupitishwa bungeni tarehe 28 Juni 2013 kwa kuwa yeye
ambaye ndiye msemaji wa kamati ameanza kutoa majibu.
Pia,
aeleze iwapo yupo tayari kumshauri Spika aruhusu kamati ya bajeti
ikutane kwa dharura wiki ijayo kufanya kazi ya kupitia matumizi ya
Serikali kwa lengo la kuanisha maeneo ambayo Serikali inaweza kubana
matumizi kwa haraka kufidia pengo la bilioni 178 zinazotafutwa kwenye
tozo hiyo ya simu. Hatua hii itawezesha kodi hiyo kuacha kutozwa bila ya
kulazimika hata kuongeza vyanzo vingine vya fedha iwapo Serikali
inasuasua kupanua wigo wa mapato.
Izingatiwe kuwa katika
kuwawakilisha wananchi ili kuepusha kutozwa kodi ya kumiliki kadi ya simu na
nyingine zenye kuongeza gharama za maisha kwa wananchi, kabla ya
kupitishwa kwa muswada wa sheria ya fedha nilichukua hatua kuanzia
bungeni katika mkutano uliopita wa Bunge.
Niliwasilisha
kwa Bunge kupitia ofisi ya Katibu wa Bunge jedwali la marekebisho ya
sheria hiyo kwa mujibu wa Kanuni ya 86 (11) ambapo pamoja na mapendekezo
mengine nilitaka kifungu katika jedwali la marekebisho la Serikali
kilichopendekeza kuanzisha ushuru huo kiondolewe.
Ikumbukwe
kwamba kwamba katika mchango wangu kwa kuzungumza bungeni nilisema
muswada wa sheria ya fedha wa mwaka 2013 ni “muswada wa majanga” ambao
utaleta athari za ongezeko la bei ya bidhaa na huduma muhimu.
Hata
hivyo, Kamati ya Bajeti chini ilikataa mapendekezo hayo, hata hivyo kwa
kuwa masharti ya kanuni za kudumu za Bunge yanakataza mbunge mwingine
kutoa taarifa za majadiliano ya ndani ya kamati sitaeleza kwa undani
yaliyojiri katika kikao cha kamati tajwa.
ANDREW CHENGE-MWEYEKITI WA KAMATI YA BUNGE YA BAJETI
Hivyo taarifa
rasmi na sababu za mapendekezo hayo kukataliwa zinaweza kutolewa na
mwenyekiti wa kamati hiyo Mh. Andrew Chenge (Mb) kwa kuulizwa kupitia
namba yake ya simu ya mkononi/kiganjani (0754782577).
Uongozi bora
na uraia mwema....
wenye uwajibikaji ni chimbuko na chachu ya ukuaji endelevu wa uchumi wa nchi na ustawi wa maisha ya wananchi.
wenye uwajibikaji ni chimbuko na chachu ya ukuaji endelevu wa uchumi wa nchi na ustawi wa maisha ya wananchi.
Kwa
ufupi nilielelezwa kwamba tayari chanzo hicho cha mapato na vingine
vilishaingizwa katika bajeti ya Serikali kwa ajili ya matumizi ya
kawaida na ya miradi ya maendeleo kwa mwaka wa fedha 2013/2014 na
kupigiwa kura ya ndio na wabunge wengi kabla ya muswada huo wa sheria ya
fedha kujadiliwa. Hivyo nilitakiwa kuwasilisha mapendekezo ya vyanzo
mbadala vya kuziba pengo litakalotokana na kufuta ushuru huo na kodi
zingine nilizopendekeza zifutwe au zipunguzwe.
Katika
muktadha huo kwa upande wa sekta ya mawasiliano pekee, nilipendekeza
vyanzo mbadala vyenye jumla ya zaidi ya bilioni 400 za kitanzania ambazo
ni zaidi ya lengo lililowekwa na Serikali bila ya kuongeza mzigo wa
gharama kwa wananchi wa kawaida. Nilitoa ushuhuda wa kitakwimu kutoka
nchi ya Ghana ambayo makampuni ya simu yanachangia asilimia 10 ya mapato
ya nchi hiyo bila kuongeza mzigo mkubwa wa gharama kwa watumiaji wa
kawaida wa huduma za simu ya kiganjani/mkononi.
Kati ya
mapendekezo niliyotoa ni pamoja na kutaka marekebisho ya Sheria ya
Mawasiliano ya njia Kieletroniki na Posta ya mwaka 2009 ili kuipa uwezo
wa kutosha Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) kufanya
ukaguzi wa uwekezaji unaofanywa na makampuni ya simu. Hata hivyo,
mapendekezo hayo yalikataliwa na kamati ya fedha chini ya uenyekiti wa
Andrew Chenge (Mb).
Ifahamike kuwa kwa kurejea masharti ya
Kanuni ya 109 (2) niliwasilisha pia katika ofisi kwa Katibu wa Bunge
kabla mjadala kuhusu muswada huo kufungwa mapendekezo ya ziada ya vyanzo
mbadala vya mapato vya kuziba pengo lililotokana na marekebisho
niliyotaka yafanyike kwa lengo la kupunguza mzigo wa gharama za maisha
kwa wananchi kutokana na ongezeko la kodi.
Marekebisho
hayo yangechangia katika kudhibiti udanganyifu unaofanywa na makampuni
mengi ya simu juu ya uwekezaji na faida wanayoipata. Marekebisho hayo
yangewezesha pamoja na mambo mengine makampuni mengi kuorodheshwa
katika soko la hisa la Dar Es Salaam na pia kudhibiti usajili wa
makampuni katika nchi zenye mfumo wa kuwezesha ukwepaji kodi (Tax
Heavens).
John Mnyika (Mb)
25 Julai 2013
0 comments:
Chapisha Maoni