Searching...
Jumanne, 30 Julai 2013

WANANCHI WA WILAYA ZA BABATI NA MWANGA WATOA MAONI KUHUSU RASIMU YA KATIBA MPYA

1.
Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Bw. Yahya Msulwa  (aliyesimama) akizungumza na Wajumbe a Baraza la Katiba la Wilaya la Halmashauri ya Mji wa Babati Mkoani Manyara wakati wa kufunga mkutano wa Baraza hilo jana Jumatatu (Julai 29, 2013). Kushoto ni Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Babati  Mjini, Bi. Christina Mndeme (kushoto).
2.
Mjumbe wa Baraza la Katiba la Hamshauri ya Mji wa Babati Mkoani Manyara, Bi. Zainab Zubery akitoa Maoni yake kuhusu Rasimu ya Katiba Mpya iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo jana Jumatatu (Julai 29, 2013).
3.
Mjumbe wa Baraza la Katiba la Hamshauri ya Mji wa Babati Mkoani Manyara, Mchungaji  Wilson Ihucha akitoa Maoni yake kuhusu Rasimu ya Katiba Mpya iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo jana  Jumatatu (Julai 29, 2013).
4.
Mjumbe wa Baraza la Katiba la Halmashauri ya Mji wa Babati Mkoani Manyara Bw. Yahya Ramadhani (kulia), akisoma nakala ya Rasimu ya Katiba Mpya ilitolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba wakati wa mkutano uliotishwa na Tume katika Halmashauri hiyo jana Jumatatu (Julai 29, 2013).
5.
Mjumbe wa Baraza la Katiba la Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga Mkoani Kilimanjaro, Bw. Bakari Mbaga akitoa maoni kuhusu Rasimu ya Katiba Mpya iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Ualimu Green Bird Wilayani humo jana (Jumatatu Julai 29, 2013).
6.
Mjumbe wa Baraza la Katiba Katiba la Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga Mkoani Kilimanjaro, Bw. Ashrafali Mruma akitoa maoni kuhusu Rasimu ya Katiba Mpya iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Ualimu Green Bird Wilayani humo jana (Jumatatu Julai 29, 2013).(PICHA NA TUME YA KATIBA)

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!