EDSON CAVAN.
Hatimaye baada ya uvumi na tetesi nyingi kwamba mchezaji nguli wa napoli na timu ya taifa ya Uruguai kwamba yupo njiani kutua kwa matajiri wa London Chelsea matajiri wengine wa ufaransa Paris Saint German PSG wameingilia kati na kuvuruga dili hilo na sasa PSG wanatarajiwa kumtangaza Cavan kuwa mchezaji wao muda wowote kuanzia sasa.
Hapo awali inasemekana Cavan alikwisha kuafikiana na Chelsea mafao yake binafsi ambapo ilikuwa alipwe paundi milioni 7.2 kwa msimu mmoja lakini PSG wamempa paundi milioni 55 kwa ajili ya huduma yake kwa kipindi chote cha mkataba wake hapo PSG
CHRISTIAN BENTEKE.
Ikionekana kama mwaka wa njaa,mikosi,shida,nuksi na kadhia mchezaji mwingine ambaye wameonyesha kumuwinda baada ya kuwakosa magwiji Lewandowski,Cavan,Rooney,Christian Benteke naye sasa asema hataki kwenda Chelsea badala yake anataka kutua Tottenham japo klabu yake ya Aston Villa imemshauri kutua Chelsea ili kupata thamani kubwa zaidi
LUIS NANI.
Mshambuliaji wa Manchester United Luis Nani anatakiwa kwa udi na uvumba na klabu tajiri ya urusi ya Anzhi Makhachkala.
Nani hatakuwa mmoja wa wachezaji wanaotarajiwa kutumiwa na kocha mpya wa Man U wanaoondoka leo jumatano kwenye mechi za maandalizi ya msimu ujao ambapo wanaenda kuweka kambi huko mashariki ya mbali pamoja na Australia.
mshambuliaji huyu kwa sasa ni majeruhi na hatoweza kwenda kwenye ziara hiyo ya wiki tatu japo tayari yupo kwenye maandalizi ya kutua Anzhi kwa kitita cha paundi milioni 12.
Baada ya miaka 20 iliyopita usiku wa jana walikutana pamoja maveterani wa Manchester UnitedDavid Beckham,Paul Scholes,Nick Butt,Ryan Giggs,Phil Neville na
Gary Neville wamekutana pamoja katika sherehe fupi ya kumbukumbu "get-together Part"
0 comments:
Chapisha Maoni