Mhe. Membe na Mhe. Al Sabah wakisaini
Mkataba wa Makubaliano kuhusu Ushirikiano katika masuala ya Siasa kati
ya Tanzania na Kuwait. Tukio hilo lilifanyika katika Hoteli ya Hyatt
Regency-Kilimanjaro Jijini Dar es Salaam tarehe 12 Julai, 2013. Kulia ni
Bw. Benedict Msuya, Afisa Mambo ya Nje.
Mhe. Membe akizungumza na Mhe. Al
Sabah (hayupo pichani) walipokutana. Wengine katika picha ni Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Mahadhi Juma
Maalim (Mb.) (wa kwanza kushoto kwa Mhe. Membe), Balozi wa Tanzania
nchini Saudi Arabia, Mhe. Prof. Abillah Omar (kulia) na Mkurugenzi wa
Idara ya Mashariki ya Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Kimataifa, Balozi Simba Yahya (kushoto)
Mhe. Al Sabah akizungumza na Mhe. Membe (hayupo pichani).
Mhe. Al Sabah akifurahia zawadi aliyokabidhiwa na Mhe. Membe.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe
(Mb.), akimkaribisha nchini Mhe. Sheikh Khalifa Al Hamad Al Sabah, Naibu
Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kuwait ambaye yupo nchini kwa
ziara ya kikazi.
Mhe.
Membe akimpatia maelekezo Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda
katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Naimi
Aziz ambaye alishiriki mazungumzo kati ya Mhe. Membe na Mhe. Al Sabah.
Mhe. Prof. Omar (katikati) na Balozi
Yahya (kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na Maafisa katika Wizara ya
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Kutoka kushoto ni Bw. Abas
Mngwali, Bw. Hassan Mwamweta na Bi. Tagie Daisy Mwakawago.Picha na Ally Kondo.
0 comments:
Chapisha Maoni