Meneja
Uhusiano wa nje wa Vodacom Tanzania, Salum Mwalim, Akizungumza na
waandishi wa habari ( Hawapo pichani) Wakati akitangaza tarehe ya
utoaji wa zawadi za ligi kuu ya Vodacom zitakazo tolewa julai 3 jijini
Dar es Salaam, Zawadi hizo ni za jumla ya shilingi Milioni 200
zitakazotolewa kwa vipengele mbalimbali kwa timu za ligi hiyo
Waandishi
wa habari wakimsikiliza meneja Uhusiano wa nje wa kampuni ya Vodacom
Tanzania Salum Mwalim ( Hayupo pichani) Wakati akitangaza tarehe ya
utoaji wa zawadi za ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara zitakazo tolewa
julai 3 jijini Dar es Salaam.
======= ======= ========
Vodacom
kukabidhi zawadi ligi kuu Julai 3 Dar es Salaam 24 Juni, 2013 .....
Wadhamini wakuu wa Ligi kuu soka Tanzania Bara Kampuni ya Vodacom
imetangaza kuwa itakabidhi zawadi kwa washindi wa ligi hiyo Julai 3
jijini Dar es salaam.
Vodacom imekuwa ikisubiri kumalizika kwa hekaheka za timu ya taifa -
Taifa Stars za kusaka nafasi ya kushiriki fainali za kombe la dunia
mwakani nchini Brazil hali iliyochelewesha tukio la kukabidhi zawadi
hizo kwa mabingwa pamoja na wote waliofanya vema katika msimu wa
2012/2013
"Tulikuwa tukisbiri wakati muafaka wa kufanya hivyo kwani tangu
kumalizika kwa ligi mwezi uliopita mwelekeo wa taifa ulikuwa ni kuipa
ari na nguvu timu yetu ya taifa katika kusaka tiketi ya kufuzu kushiriki
fainali za kombe la dunia mwakani nchini Brazil." Alisema Meneja
Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim.
Mwalim amesema maandalizi yote ya zoezi hilo yamekamilika kwani
hakukuwa na sababu nyingine ya kutokabidhi zawadi mara tu baada ya ligi
kumalizika zaidi ya timu ya taifa - taifa stars.
Mwalim amesema hafla ya utoaji wa zawadi inahitaji ushiriki wa wadau
mbalimbali wa soka nchini wakiwemo wachezaji wa vilabu ambao miongoni
mwao wamo kwenye kikosi cha Stars, viongozi wa TFF na walimu wa timu ya
taifa ambao wote hao kwa pamoja walikuwa na jukumu moja tu la
kuhakikisha Stars inafuzu kwenda Brazil na hivyo isngekuwa vema kuingiza
maandalizi ya jambo jingine katikati ya juhudi hizo.
Mwalim ametumia nafasi hiyo kuvishukuru vilabu pamoja na Shirikisho la
Soka - TFF na kamati ya ligi kwa uvumulivu wao wakati wote ambapo
Vodacom ikisubiri kupatikana kwa muda mufaka wa kukabidhi zawadi.
"Tendo la kukabidhiwa zawadi ni moja ya matendo makuu kabisa kwa yeyote
anaeshinda, tumeona uvumilivu mkubwa na wenzetu walituelewa wakati
tulipowashauri kutoa nafasi kwa Stars bila kuharibu concetratiuon ya
taifa. Tumeonesha umoja wetu."
Mbali ya mabingwa timu ya Yanga ambayo watakabidhiwa kitita cha fedha
cha Sh 70 Milioni zinahusisha pia zawadi za wachezaji na wadau wengine
mmoja mmoja walioonesha umahiri kwenye maeneo yao.
Vodacom itakabidhi zawadi za fedha taslimu takribani Sh. 200 Milioni
kwa mabingwa Yanga na Azam, Simba na Kagera Sugar zilizoshika nafsi ya
pili hadi ya nne.
Wengine
watakaonufaika na zawadi za fedha ni Mlinda mlango bora, mwamuzi bora,
mwalimu bora, timu iliyoonyesha nidhamu na mfungaji bora. Vodacom
imekuwa ikiidhamini ligi kuu ya soka ya Tanzania bara kwa zaidi ya
misimu mitano sasa huku ikiiwezesha ligi hiyo kuimarika na kuwa ya
ushindani kadri miaka inavyosonga mbele.
0 comments:
Chapisha Maoni