Mkuu
wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Rehema Nchimbi akimkaribisha Spika wa Bunge la
Oman Mhe. Sheikh Khalid Bin Hilal Bin Nasir Al Maawali mara baada ya
kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Dodoma jana.
Kaminisha
wa Tume ya Utumishi ya Bunge Mhe. Abdulkarim Shah akimkaribisha Spika
wa Bunge la Oman Mhe. Sheikh Khalid Bin Hilal Bin Nasir Al Maawali mara
baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Dodoma jana.
Naibu
Spika Mhe. Job Ndugai akimtambulisha Katibu wa Bunge. Dkt. Thomas
Kashililah kwa Spika wa Bunge la Oman Mhe. Sheikh Khalid Bin Hilal Bin
Nasir Al Maawali alipowasili Dodoma jana.
Spika
wa Bunge Mhe. Anne Makinda akimkaribisha Spika wa Bunge la Oman Mhe.
Sheikh Khalid Bin Hilal Bin Nasir Al Maawali mara baada ya kuwasili
katika viwanja vya Bunge Dodoma ambapo anafanya ziara ya kibunge ikiwa
ni pamoja na kusaini makubaliano ya ushirikiano baina ya mabunge haya
mawili.
Spika
wa Bunge Mhe. Anne Makinda pamoja na Spika wa Bunge la Oman Mhe. Sheikh
Khalid Bin Hilal Bin Nasir Al Maawali wakisaini mikataba ya makubaliano
ya ushirikiano baina ya mabunge haya mawili.
Wakibadilishana mikataba ya Makubaliano.
Picha ya Pamoja Ujumbe wa Spika wa Bunge la Oman na Wajumbe wa Tume ya Utumishi ya Bunge la Tanzania.
Spika wa Bunge la Oman Mhe. Sheikh Khalid Bin Hilal Bin Nasir Al Maawali akiwa na ujumbe wa Wabunge toka Oman yupo hapa nchini kwa ziara ya kikazi ya siku sita ambapo pamoja na mambo mengine amesaini mkataba wa uanzishwaji wa ushirikiano wa Bunge la Tanzania na Bunge la Oman katika Maswala mbalimbali. Picha zote na Owen Mwandumbya wa Bunge

PICHA NA DEMASHO BLOG.
0 comments:
Chapisha Maoni