Rais wa Amerika Barack Obama akiongea awali. Picha/AFP
TANZANIA
itakuwa nchi ya mwisho ya Afrika kutembelewa na Obama baada ya Senegal
na Afrika Kusini.
Mara atakapowasili na ndege yake kubwa ya Air Force
One, Rais Obama atazindua barabara mpya katika upande wa Mashariki wa
geti la kuingia Ikulu.
Rais Obama,
ambaye atafuatana mkewe Michelle pia siku hiyohiyo atazungumza kwa
nyakati tofauti na wafanyabiashara kutoka nchi za Afrika na Marekani
kwenye Hoteli ya Hyatt Regency, Dar es Salaam.
“Pia amepanga kuzungumza na maofisa wa Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania,” ilisema taarifa ya Maelezo.
Baada ya shughuli hiyo, Rais Obama atahudhuria dhifa ya taifa atakayoandaliwa Ikulu na mwenyeji wake, Rais Jakaya Kikwete.
Siku
itakayofuata ataweka shada la maua kwenye sehemu ulipokuwa Ubalozi wa
Marekani ikiwa ni kumbukumbu ya watu waliofariki katika shambulizi la
bomu mwaka 1998. Pia atatembelea mitambo ya kufua umeme ya Kampuni ya
Symbion na atatoa hotuba akizungumzia mikakati ya Marekani ya kulisaidia
Bara la Afrika kuzalisha nishati ya umeme.
“Tanzania ni
mshirika muhimu wa Marekani,” alisema Ofisa wa Ikulu ya Marekani, Ben
Rhodes wakati alipozungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki
katika Ikulu ya Marekani kuhusu ratiba ya ziara ya Obama barani Afrika.
Staftahi
Pia mke wa
Obama atakuwa na ratiba yake. Julai Mosi, atapata staftahi na mwenyeji
wake, Salma Kikwete katika ofisi za Taasisi ya Wanawake na Maendeleo
(Wama), Dar es Salaam.
Pia
atatembelea sehemu ubalozi wa zamani wa Marekani na baadaye atashuhudia
onyesho la utamaduni la Kikundi cha Baba wa Watoto, ambacho kinajumuisha
watoto wa mitaani wenye umri kuanzia miaka mitano hadi 18 kwenye
Makumbusho ya Taifa.
Julai 2,
atahudhuria mkutano na wake wa marais wa nchi za Afrika ambao pia
utahudhuriwa na mke wa Rais wa zamani wa Marekani, George Bush, Laura.
0 comments:
Chapisha Maoni