RAIS WA BRAZIL BI.DILMA ROUSSEFF
Rais wa Brazil Dilma Rousseff amemaliza ukimya aliokuwa nao juu ya maandamano makubwa ya ghasia, akisema kuwa maandamano ya amani ni sehemu ya demokrasia imara lakini ghasia haziwezi kuvumilika.
Bi Dilma Ameahidi kuimarisha huduma za umma na kufanya mazungumzo na viongozi wa maandamano,lakini bado haifahamiki hasa nani anaweza kuwakilisha makundi
makubwa ambayo hayana uongozi ya waandamanaji wanaoingia mitaani,
wakitoa hasira zao dhidi ya huduma mbovu za umma licha ya
mzigo mkubwa wa kodi unaowakabili.
0 comments:
Chapisha Maoni