Mzee Yasin
Maluzuku akiongea na wandishi wa habari ofisini kwake leo hii .
Mzee Yasin
Maluzuku akionyesha sehemu yenye ufa katika ofisi yake
Hapa Mzee Yasin
Maluzuku akiwa mbele ya nyumba yake
Mzee Yasin
Maluzuku
Na Amon Mtega,Songea.
MWASISI
wa chama cha mapinduzi CCM wa Kata ya Misufini Manispaa ya Songea
mkoani Ruvuma mzee Yasin Maluzuku amelalamikia uchakavu wa nyunba yake
ambayo ipo
hatarini kuanguka kufuatia uchakavu wa muda mrefu uliotokana na
kutokufanyiwa
matengenezo pamoja na nyumba hiyo kutumika
kama ofisi ya chama cha mapinduzi tawi la Msikitini pia hawajapewa
msaada
wowote na chama pamoja na kukitumikia
tangu enzi za kupigania uhuru wa Tanganyika.
Mzee Maluzuku akiongea na mtandao huu nyumbani kwake alisema
kuwa yeye amekitumikia chama hicho kwa
muda mrefu tangu alipokutana na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wakati wa
harakati za kupigania uhuru wa nchi hii mwaka 1955 na kuwa ameshashika nyadifa mbali
mbali za kiuongozi mpaka alipoamua
kustaafu kwa sababu ya umri mwaka 2012 lakini chama bado hakijaonesha kuwajali
kwa dhati wazee na hasa waasisi wa uhuru wa taifa hili.
Amesema kuwa mwalimu
Nyerere wakati akipita kuelekea Nyasa alimuona mzee maluzuku kwenye kijiji
kilichopo karibu na Nyasa na kumwambia ajiunge na chama cha TANU ndipo mzee huyo alikubali na kuanza kazi ya kusaka uhuru
na alianza kazi hiyo kwa kubeba mizigo ya Mwalimu alipokuwa akifanya ziara
Ruvuma.
Aidha pamoja na kupumzika
kushika madaraka ndani ya chama hicho mzee huyo alisema kuwa ameamua kugawa
chumba kimoja ndani ya nyumba yake kitumike
kama ofisi ya CCM tawi la Msikitini baada ya kuona tawi hilo linahangaika
mahali pa kufanyia kazi za kiofisi licha ya nyumba hiyo kuwa na dalili zote za
kuanguka.
Maluzuku akiongelea
upande wa rasimu ya katiba mpya iliyotoka sasa ambayo inaendelea kujadiliwa na
wananchi mbali mbali amedai kuwa rasimu hiyo ni nzuri lakini inatakiwa ifanyiwe
marekebisho madogo madogo hasa kwa upande wa muundo wa serikali tatu kwa sababu
muundo huo utaligharimu Taifa na kuwa ulinzi wake utakuwa mgumu zaidi.
0 comments:
Chapisha Maoni