MHESHIMIWA JOSEPH MBILINYI MBUNGE WA MBEYA-CHADEMA.
Taarifa zilizoufikia mtandao huu wa kijamii zinasema mheshimiwa Mbilinyi au Sugu kama anavyofahamika na wengi amepata ajali mbaya mchana wa leo lakini yupo salama ila gari alilokuwa akisafiria limeharibika vibaya...akizungumza na MCHOME BLOG dereva wa mheshimiwa Mbilinyi bwana Mkoloni amesema ni kweli SUGU amepata ajali lakini yeye(Mkoloni)hakuwa naye alikua anaendesha mwenyewe na bado juhudi za kupata habari zaidi kuhusiana na ajali hiyo zinaendelea kufanywa na bwana mkoloni....taarifa zaidi kuhusiana na ajali hii na picha utaziona humu pindi zikitufikia.
0 comments:
Chapisha Maoni