Searching...
Jumatatu, 17 Juni 2013

HALIMA MDEE Vs JACKLINE WOLPER SABA SABA KUONYESHANA KAZI-MDEE AINGIA KAMBINI KUJIFUA NA MPAMBANO HUO



Mbunge wa Kawe (Chandema), Halima Mdee ameanza maandalizi yake ya pambano la ngumi dhidi ya staa wa Bongo Movies, Jacqueline Wolper.

Pambano la wakali hao litafanyika Julai 7, siku ya Sabasaba katika Tamasha la Matumaini kwenye Uwanja we Taifa jijini Dar es Salaam.


Halima Mdee amekuwa akiendelea na mazoezi yake chini ya Mbunge wa CCM, Idd Azzan ambaye anaamini bondia wake siku hiyo atatoa funzo kwa Wolper.



Katika tamasha hilo mwaka jana Wolper alionyesha uwezo kuliko Wema Sepetu katika pambano lao lililosisimua.

Lakini Mdee ametamba kumpoteza Wolper katika pambano lao hilo la Julai 7.
Mdee anaendelea na mazoezi mjini Dodoma, wakati Wolper anaendelea na mazoezi jijini Dar es Salaam.
kwa hisani ya SALEHE JEMBE BLOG

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!