Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal,
akiwahutubia washiriki wa Majadiliano ya Kitaifa ya Ushirikiano kwa
manufaa ya Wote, wakati akifungua rasmi Majadiliano hayo yaliyoanza leo
Juni Mosi, 2013 kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.
Katibu
Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue, akizungumza machache kabla ya kumkaribisha
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mary Nagu, kumkaribisha Mhe. Makamu wa
Rais.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu ( Uwekezaji na Uwezeshaji) Dkt. Mary Nagu,
akisoma Hotuba yake kabla ya kumkaribisha Makamu wa Rais kufungua
Majadiliano hayo.
Sehemu
ya washiriki wa Majadiliano hayo, wakimsikiliza Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, wakati
akisoma hotuba yake ya ufunguzi wa majadiliano hayo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal,
akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Majadiliano ya Kimataifa
ya Ushirikiano kwa Manufaa ya wote, baada ya kufungua majadiliano hayo
leo. Picha na OMR.







0 comments:
Chapisha Maoni